Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, November 9, 2013

Nyama hatari yauzwa nchini



 
Sehemu ya Machinjio ya Vingunguti jijini Dar es Salaam. PICHA | IBRAHIM YAMOLA

Dar es Salaam. Afya za maelfu ya walaji wa nyama katika Jiji la Dar es Salaam zipo hatarini baada ya kubainika kuwa nyama inayochinjwa katika machinjio mengi haifai kwa matumizi ya binadamu.

Hali hiyo inatokana na mifugo kuchinjwa bila kufuata taratibu za afya na kuingizwa sokoni, ikiwamo nyama hizo kutokaguliwa na wataalamu wa mifugo kabla ya kuchinjwa.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili katika machinjio mbalimbali ya maeneo ya Vingunguti, Ukonga, Kimara Suka, Tegeta na Mbagala, umebaini taratibu za kuchinja hazifuatwi huku maeneo hayo yakiwa yamejaa uchafu.

Mwandishi wa habari hizi alifika katika machinjio hayo kwa nyakati tofauti alfajiri na kushuhudia ukiukwaji wa taratibu za uchinjaji, ambapo nyama zinatupwa ovyo, kwenye mazingira hatari, huku nyingine zikiwekwa karibu na  madimbwi ya maji machafu.

TMB: Machinjio hayafai

Alipotafutwa kuzungumzia hali hiyo, Msajili wa Bodi ya Nyama Tanzania (TMB),  Suzana Kiango alisema kuwa machinjio yote yaliyopo jijini Dar es Salaam hayafai.

Kiango alisema kuwa endapo kila mmoja aliye na jukumu la kusimamia sheria na kanuni za uchinjaji nyama akizitekeleza, basi machinjio yote ya jijini Dar es Salaam yanastahili kufungwa. Suzana alisema kuwa Sheria ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) namba 1 ya mwaka 2003 na Sheria ya Magonjwa ya Mifugo Namba 17 ya mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2007 zote kwa pamoja hazisimamiwi ipasavyo.

Anataja baadhi ya sifa ambazo machinjio yanatakiwa kuwa nazo ni mabomba ya kutoa maji safi na salama, maabara ndogo, mifereji ya kutolea maji machafu, mabanda ya kutunza mifugo kabla ya kuchinjwa na chumba cha kuhifadhia nyama kabla ya mkaguzi kuifanyia uchunguzi.

“Hayo ni baadhi tu, yote hayo hayazingatiwi na TMB tunasema kwamba iwapo sheria na kanuni zitafuatwa, hakika machinjio yote ya Dar es Salaam yatafungwa,” anasema Suzana na kuongeza:

“Mifugo inapochinjwa inashauriwa iwe imepoteza fahamu kabla ya kukatwa shingo ili kuwezesha damu kutoka yote katika misuli, lakini haya hayazingatiwi na uchinjaji unafanyika chini, kila kitu kinafanyika chini, jambo ambalo ni kinyume na kanuni za uchinjaji.”

Kauli za Wataalamu

Mkaguzi wa nyama ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini alisema kuwa, asilimia kubwa ya nyama inayoliwa na wakazi wa Jiji la Dar es Salaam siyo salama kiafya kutokana na uchinjaji wake kutofuata taratibu zinazokubaliwa.chanzo mwanainchi

No comments:

Post a Comment