Sehemu ya Machinjio ya Vingunguti jijini Dar es Salaam. PICHA | IBRAHIM YAMOLA
Dar es Salaam. Afya za maelfu ya walaji wa nyama katika Jiji la Dar es Salaam zipo hatarini baada ya kubainika kuwa nyama inayochinjwa katika machinjio mengi haifai kwa matumizi ya binadamu.
Dar es Salaam. Afya za maelfu ya walaji wa nyama katika Jiji la Dar es Salaam zipo hatarini baada ya kubainika kuwa nyama inayochinjwa katika machinjio mengi haifai kwa matumizi ya binadamu.
Hali hiyo inatokana na mifugo kuchinjwa bila
kufuata taratibu za afya na kuingizwa sokoni, ikiwamo nyama hizo
kutokaguliwa na wataalamu wa mifugo kabla ya kuchinjwa.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili katika
machinjio mbalimbali ya maeneo ya Vingunguti, Ukonga, Kimara Suka,
Tegeta na Mbagala, umebaini taratibu za kuchinja hazifuatwi huku maeneo
hayo yakiwa yamejaa uchafu.
Mwandishi wa habari hizi alifika katika machinjio
hayo kwa nyakati tofauti alfajiri na kushuhudia ukiukwaji wa taratibu za
uchinjaji, ambapo nyama zinatupwa ovyo, kwenye mazingira hatari, huku
nyingine zikiwekwa karibu na madimbwi ya maji machafu.
TMB: Machinjio hayafai
Alipotafutwa kuzungumzia hali hiyo, Msajili wa
Bodi ya Nyama Tanzania (TMB), Suzana Kiango alisema kuwa machinjio yote
yaliyopo jijini Dar es Salaam hayafai.
Kiango alisema kuwa endapo kila mmoja aliye na
jukumu la kusimamia sheria na kanuni za uchinjaji nyama akizitekeleza,
basi machinjio yote ya jijini Dar es Salaam yanastahili kufungwa. Suzana
alisema kuwa Sheria ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) namba 1 ya
mwaka 2003 na Sheria ya Magonjwa ya Mifugo Namba 17 ya mwaka 2003 na
kanuni zake za mwaka 2007 zote kwa pamoja hazisimamiwi ipasavyo.
Anataja baadhi ya sifa ambazo machinjio yanatakiwa
kuwa nazo ni mabomba ya kutoa maji safi na salama, maabara ndogo,
mifereji ya kutolea maji machafu, mabanda ya kutunza mifugo kabla ya
kuchinjwa na chumba cha kuhifadhia nyama kabla ya mkaguzi kuifanyia
uchunguzi.
“Hayo ni baadhi tu, yote hayo hayazingatiwi na TMB
tunasema kwamba iwapo sheria na kanuni zitafuatwa, hakika machinjio
yote ya Dar es Salaam yatafungwa,” anasema Suzana na kuongeza:
“Mifugo inapochinjwa inashauriwa iwe imepoteza
fahamu kabla ya kukatwa shingo ili kuwezesha damu kutoka yote katika
misuli, lakini haya hayazingatiwi na uchinjaji unafanyika chini, kila
kitu kinafanyika chini, jambo ambalo ni kinyume na kanuni za uchinjaji.”
Kauli za Wataalamu
Mkaguzi wa nyama ambaye aliomba jina lake
lisiandikwe gazetini alisema kuwa, asilimia kubwa ya nyama inayoliwa na
wakazi wa Jiji la Dar es Salaam siyo salama kiafya kutokana na uchinjaji
wake kutofuata taratibu zinazokubaliwa.chanzo mwanainchi
No comments:
Post a Comment