Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongozwa na Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kukagua daraja la Mwanhuzi lililoko Meatu Mkoani Simiyu
Muonekano
wa Daraja la Mwanhuzi.
Ahadi
ya ujenzi wa daraja la Mwanhuzi katika wilaya ya Meatu mkoani Simiyu imetimia
baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete kulifungua
rasmi daraja hilo ambalo ujenzi wake umekamilika na tayari limeanza hutumika.
Awali
kabla ya kulifungua daraja hilo Rais Kikwete aliwaasa wananchi wa eneo hilo la
Mwanhunzi pamoja na watumiaji wengine kulitunza daraja hilo ili liweze kudumu
kwa muda uliokusudiwa na hivyo kuhakikisha panakuwepo huduma hiyo muhimu ya
usafiri kati ya Wilaya ya Meatu na Mikoa ya jirani ya Arusha na Singida.
‘Ninawasihi
mlitunze daraja hili na asije akatokea mtu kwenda kuanza kukata vyuma au
kunyofoa vifaa vingine vya daraja kwani kwa kufanya hivyo mtalidhoofisha ubora
wake na hatimaye kuharibika kabisa tukajikuta tunarusi katika kero ya usafiri
katika eneo hili kama ilivyokuwa hapo awali kabla ya kujengwa kwa daraja”
Alisisitiza Rais kikwete .
Aidha,
Mhe. Rais aliongeza kuwa atahakikisha katika kipindi cha miaka miwili
kilichobakia akishirikiana na Waziri Magufuli watahakikisha wanafikisha sehemu
nzuri ahadi zote za miradi ya barabara katika wilaya hiyo na mkoa wa Simuyu kwa
ujumla.
Daraja
la hilo lenye urefu wa meta 40 ni kiungo muhimu cha usafiri kuvuka mto Mwanhuzi
ambako barabara kuu inayo tokea Kolandoto mkoani Shinyanga kupitia Lalago
katika mkoa wa Simiyu na kuelekea mikoa ya Singida na Arusha.
Awali
wakati akimkaribisha Rais, Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
alielezea kuwa usanifu pamoja na usimamizi wa daraja hilo umefanywa na Wakala
wa Barabara Nchini (TANROADS) kwa gharama ya Shilingi milioni 13.45 na ujenzi
wake umetekelezwa kwa awamu mbili.
”Kukamilika
kwa mradi huu ni moja ya ushahidi unaothibitisha kuwa ahadi ulizotoa kwa
wananchi zinakamilika popote bila kuangalia itikadi za vyama au watu” alisema
Waziri Magufuli
Waziri
Magufuli alifafanua kuwa awamu ya kwanza ya ujenzi wa daraja hilo ilikamilika
mwezi Agosti mwaka 2013 ikiwa imejengwa na Mkandarasi M/S Pet Cooperation
kutoka Kahama kwa gharama ya Shilingi milioni 355.58.
Awamu
ya pili ya mradi huu ambazo zilianza mwezi Agosti 2013 na kukamilika nwezi
Oktoba 2013 zilijumuisha ujenzi wa kingo za daraja. Kazi hizo zillitekelezwa
chini ya usimamizi wa Ofisi ya Meneja wa Tanroads mkoa wa Simiyu mara baada ya
mkoa huo mpya kuanzishwa. Awamu hii ya pili ilitekelezwa na Kampuni ya Ms
Tolerance Engineering Ltd ya Dar es Salaam kwa gharama ya Shilingi milioni
97.55.
Fedha hizo zote
zilizotumika katika ujenzi wa awamu zote mbili pamoja na usimamizi ambazo ni
jumla ya Shilingi milioni 455.58 zimetolewa na Mfuko wa Barabara (Roads)
No comments:
Post a Comment