Serikali yabariki TANESCO kupandisha gharama za umeme
Naibu Waziri wa umeme, Mh George Simbachawene, amesema kwamba serikali imekubali TANESCO waongeze gharama za umeme kwa 68% kama walivyokuwa wameomba. Alisema hayo wakati akiongea katika kipindi cha Kumepambazuka kupitia Radio One leo asubuhi. Amsema kwamba hata kama TANESCO wakiongeza gharama za umeme hadi kufikia Tsh 800 kwa unit bei hiyo ni nafuu kuliko gharama za kununua mafuta ya taa.
Mh Simbachawene ametahadharisha kwamba kama mtu ataona kwamba gharama za umeme ni kubwa, basi akawashe kibatari au akae gizani.
Source: Kumepambazuka, Radio One NA JF
No comments:
Post a Comment