Mshindi
wa tuzo ya Daudi Mwangosi Absalom Kibanda ambae ni mwenyekiti wa
jukwaa la wahariri akibembelezwa na mkewe baada ya kuangua kilio
ukumbini mara baada ya kutangazwa mshindi wa tuzo hiyo Jana jijini
Mwanza.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo ya kukabidhi tuzo ya Daudi
Mwangosi Bw Tido Mhando wa tatu kulia akimkabidhi mshindi mfano
wa hundi ya Tsh milioni 10 Absalom Kibanda tuzo yenye thamani ya
Tsh milioni 10,0000 katikati ni mjane wa Mwangosi Itika Mwangosi wa
kwanza kushoto ni makamu wa rais wa UTPC Jane Mihanji na rais wake
Keneth Simbaya.
----
Na Abdulaziz video,Mwanza
Mhariri mtendaji wa Kampuni ya New Habari Absalom Kibanda leo
amekabidhiwa tuzo ya Uandishi wa kishujaa na Utumishi uliotukuka ya
Marehemu Daud Mwangosi baada ya Mhariri huyo kukumbwa na tukio la
uvamizi na kisha kutobolewa jicho na watu wasiofahamika Machi 6 mwaka
huu. Kabla ya makabidhiano ya tuzo hiyo wadau wote wa habari wakasimama na kisha kuimba wimbo maalumu wa kumuenzi Marehemu Daud Mwangosi.
Mhariri mtendaji wa Kampuni ya New Habari Absalom Kibanda leo
amekabidhiwa tuzo ya Uandishi wa kishujaa na Utumishi uliotukuka ya
Marehemu Daud Mwangosi baada ya Mhariri huyo kukumbwa na tukio la
uvamizi na kisha kutobolewa jicho na watu wasiofahamika Machi 6 mwaka
huu. Kabla ya makabidhiano ya tuzo hiyo wadau wote wa habari wakasimama na kisha kuimba wimbo maalumu wa kumuenzi Marehemu Daud Mwangosi.
Akizungumza na wadau wa habari Jijini Mwanza. Baada ya
makabidhiano hayo mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi
Communications Tido Mhando amewahimiza waandishi wa habari kuendelea
kupambana katika jitihada za kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya
Taifa. Kutokana na umuhimu wa tuzo hii ya Marehemu Daud Mwangosi
aliyeuwawa kwa kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu la machozi
lililolipuliwa visivyo September 2 mwaka jana kijijini nyololo mkoani
Iringa Mhando akatumia fursa hii kulaani vikali vitendo vya kuminya
uhuru wa habari vinavyofanywa na baadhi ya viongozi nchini.
Baada ya kibanda kukabidhiwa tuzo hiyo pamoja na hundi ya shilingi
millioni kumi akawapa moyo wa ujasiri waandishi wa habari kote nchi wa
kutonyamazishwa wakati wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao licha ya kuwepo changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo zikiwemo za
vitisho.
Kutokana na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya habari nchini wadau wa habari wakiwemo wakongwe katika fani hii hawakubaki nyuma kuelezea mitazamo yao kuhusu uelekeo wa sekta hii. Tuzo za uandishi wa kishujaa na utumishi uliotukuka ya Marehemu Daud Mwangosi itakuwa ikitolewa kila mwaka ili kutambua michango mbalimbali inayotolewa na waandishi wa habari katika kutekeleza majukumu yao ya kikazi
No comments:
Post a Comment