Pages

Saturday, November 9, 2013

Taswira:Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006), Absalom Kibanda aangua kilio baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya Uandishi wa Habari Uliotukuka ya Daudi Mwangosi.


 Mshindi  wa  tuzo ya Daudi Mwangosi Absalom Kibanda ambae ni mwenyekiti wa jukwaa la  wahariri akibembelezwa na mkewe  baada ya  kuangua kilio ukumbini mara baada ya kutangazwa mshindi  wa tuzo hiyo  Jana  jijini Mwanza.
 Mgeni  rasmi katika hafla  hiyo ya kukabidhi tuzo ya Daudi Mwangosi Bw  Tido Mhando  wa tatu  kulia  akimkabidhi mshindi  mfano  wa hundi ya Tsh milioni 10  Absalom Kibanda tuzo  yenye  thamani ya Tsh  milioni 10,0000 katikati ni mjane  wa Mwangosi  Itika Mwangosi  wa kwanza  kushoto ni makamu wa rais wa UTPC Jane Mihanji na  rais  wake  Keneth Simbaya.
----
Na Abdulaziz video,Mwanza
Mhariri mtendaji wa Kampuni ya New Habari Absalom Kibanda leo
amekabidhiwa tuzo ya Uandishi wa kishujaa na Utumishi uliotukuka ya
Marehemu Daud Mwangosi baada ya Mhariri huyo kukumbwa na tukio la
uvamizi na kisha kutobolewa jicho na watu wasiofahamika Machi 6 mwaka
huu.  Kabla ya makabidhiano ya tuzo hiyo wadau wote wa habari wakasimama na kisha kuimba wimbo maalumu wa kumuenzi Marehemu Daud Mwangosi. 
Akizungumza na wadau wa habari Jijini Mwanza. Baada ya makabidhiano hayo mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Tido Mhando amewahimiza waandishi wa habari kuendelea kupambana katika jitihada za kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Taifa. Kutokana na umuhimu wa tuzo hii ya Marehemu Daud Mwangosi aliyeuwawa kwa kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu la machozi lililolipuliwa visivyo September 2 mwaka jana kijijini nyololo mkoani Iringa Mhando akatumia fursa hii kulaani vikali vitendo vya kuminya uhuru wa habari vinavyofanywa na baadhi ya viongozi nchini. 

Baada ya kibanda kukabidhiwa tuzo hiyo pamoja na hundi ya shilingi
millioni kumi akawapa moyo wa ujasiri waandishi wa habari kote nchi wa
kutonyamazishwa wakati wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao licha ya kuwepo changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo zikiwemo za
vitisho.

Kutokana na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya habari nchini wadau wa habari wakiwemo wakongwe katika fani hii hawakubaki nyuma kuelezea mitazamo yao kuhusu uelekeo wa sekta hii. Tuzo za uandishi wa kishujaa na utumishi uliotukuka ya Marehemu Daud Mwangosi itakuwa ikitolewa kila mwaka ili kutambua michango mbalimbali inayotolewa na waandishi wa habari katika kutekeleza majukumu yao ya kikazi

No comments:

Post a Comment