Katibu
wa chama cha CHADEMA wilaya ya Chunya,Bwa.Bryson Mwasimba akionesha
kadi yake ya chama hicho akiirejesha kwa chama cha CCM,mara baada ya
kuachia ngazi,kwenye mkutano wa hadhara uliofanywa na Katibu Mkuu wa
CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana,uliofanyika kwenye kata ya Lupa Tinga
Tinga,Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.Ndugu Kinana na ujumbe wake yuko
mkoani Mbeya kwenye ziara kukagua utekelezaji wa Ilani ya chama,kukagua
miradi mbalimbali ya chama na wananchi sambamba na kusikiliza matatizo
ya wananchi na namna ya kuyatafutia ufumbuzi.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akimkabidhi kadi ya chama cha
CCM,Katibu wa chama cha CHADEMA Wilayani Chunya,Bwa.Bryson Mwasimba
aliyeamua kujiuzuru wadhifa wake mapema leo na kurejea CCM,huku umati
mkubwa wa watu uliofika kwenye mkutano wa hadhara ukishangilia kwa
mayowe na miluzi,uliofanywa na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman
Kinana,uliofanyika kwenye kata ya Lupa Tinga Tinga,Wilaya ya Chunya
mkoani Mbeya.
Bwa.Bryson Mwasimba akionesha kadi ya CCM mara baada ya kutangaza kuachia ngazi CHADEMA.
Bwa.Bryson
Mwasimba akizungumza mbele ya wananchi na wanachama wa CCM kuhusiana na
kuachia ngazi kwake na kurejea chama cha CCM mapema leo.CHANZO MICHUZI JR
No comments:
Post a Comment