Msanii
wa kundi la Tip Top Connection Khalid Ramadhan aka Tunda Man, alikuwa
ni miongoni mwa watu waliokuwa wanamiliki silaha za moto (bastola), kitu
kilichofahamika na kuandikwa na baadhi ya vyombo vya habari mapema
mwaka huu.
Tunda
amesema kwa sasa hamiliki tena bastola, sababu aliamua kuisalimisha
silaha hiyo aliyokuwa anamiliki kutokana na masharti mengi ya kuimiliki.
“Mimi
imenishinda mpaka nimerudisha, Kwasababu watu wengi walikuwa wanajua
mimi nilikua na bunduki halafu maneno yakawa mengi”. Alisema Tunda leo
katika kipindi cha XXL cha Clouds FM
Tunda amesema kati ya masharti yaliyomshinda ni pamoja na aina ya mavazi anayotakiwa kuyavaa mtu anayeimiliki .
“Kuna
mavazi unatakiwa uvae kidogo, mavazi ya kipapaa yale, sometimes
unatakiwa uwe nayo muda wote, kuna vitu vingi…watu wasijue kwahiyo watu
washajua watu kibao kuwa mimi nina ile, afu kuna watu wanazitafuta zile
ili wafanyie mambo yao”.
Mwezi wa pili mwaka huu gazeti la Ijumaa liliandika habari isemayo ‘SOO LA BASTOLA, TUNDA MAN AKIONA CHA MOTO’.
Hiki ndicho kilichoandikwa katika gazeti hilo:
‘TABIA
ya baadhi ya mastaa kuonyeshaonyesha bastola hadharani kimemtokea puani
‘memba’ wa Kundi la Tip Top Connection, Khalid Ramadhani ‘Tunda Man’
baada ya hivi karibuni kuitwa na jeshi la polisi na kuhenyeshwa.
Akizungumza
na Ijumaa hivi karibuni Tunda Man alisema makala iliyotoka kwenye
gazeti ndugu na hili la Ijumaa Wikienda ikieleza jinsi baadhi ya wasanii
wanavyozianika silaha kiholela imemfanya akione cha moto kwani wakati
akizungumza na mwandishi wetu alikuwa Kituo cha Polisi cha Kati
(Central) akihojiwa.
“Kwanza
naomba nikwambie kuwa hakuna kitu ambacho kimenikosesha amani leo
(Jumatatu) kama hii habari yako uliyoandika kwenye gazeti, hivi
ninavyoongea na wewe niko ‘sentro’ nikihojiwa, kiukweli sina amani,”
alisema Tunda Man.
Hivi
karibuni msanii wa muziki, Aboubakar Chende ‘Dogo Janja’ alinaswa akiwa
na bastola na alipoulizwa ni ya nani alidai ni ya Tunda Man hivyo kumpa
msala mwenzake’.
SOURCE: GLOBAL PUBLISHERS
No comments:
Post a Comment