AZAM FC ina utaratibu wa kuwaweka wachezaji wawili wawili katika vyumba vya kambi yake iliyopo Chamazi Mbagala jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo hali ni tofauti kwa wachezaji Kone
Muhamad, Balou na Kipre Tchetche ambao wanaishi chumba kimoja kutokana
na tatizo la lugha.
Kocha wa Azam, Joseph Omog amependekeza timu yake
iweke kambi Azam Complex, katika eneo ambalo uwanja wa mazoezi upo mita
chache kutoka vilipo vyumba vya wachezaji.
Kone, Balou na Tchetche wenyewe wanaishi chumba
kimoja kwa kuwa wote wanazungumza Kifaransa kwa kuwa kwao Ivory Coast
ndiyo lugha ya taifa.
Awali chumba hicho kilikuwa kinatumiwa na pacha
Balou na Tchetche ambao wanamudu pia kuzungumza Kingereza, lakini
aliposajiliwa Kone, Novemba mwaka jana wanalazimika kuishi naye chumbani
humo.
“Kone hawezi kuzungumza lugha nyingine zaidi ya
Kifaransa, anashindwa kuwasiliana na wachezaji wengine katika mazingira
ya nje ya uwanja. Tupo naye hapa chumbani ili angalau tumfundishe
Kingereza ili akimudu naye aweze kuishi na wachezaji wengine,” Tchetche
aliliambia Mwanaspoti chumbani humo.
Akizungumza na Mwanaspoti kwa msaada wa Tchetche,
Kone alisema anafurahia maisha ya Tanzania, lakini changamoto ya lugha
inampa wakati mgumu.
“Nazungumza Kifaransa tu, na ninaoweza kuzungumza
nao hapa ni Balou na Tchetche labda na kocha, lakini wachezaji wengine
ni tatizo, nikiweza kuzungumza Kingereza nitaenda chumba kingine,”
alisema Kone.
Akizungumzia hali hiyo, meneja wa Azam, Jemedari
Said alisema wamemkubali Kone kuishi chumba kimoja na raia wenzake wa
Ivory Coast ili kupata muda wa kujua Kingereza ili aweze kujichanganya
wachezaji wengine.
“Hata Tchetche alipofika hapa alikuwa anakaa na
Ibrahim Shikanda, alipojua Kingereza akajichanganya na wengine.
Alipokuja Balou akaishi na Tchetche na hadi sasa wapo pamoja,” alisema
Jemedari.CHANZO MWANASPOTI
No comments:
Post a Comment