Pages

Friday, January 24, 2014

Mawaziri wafanya makabidhiano ya wizara ya afya na ustawi wa jamii

DSC_1613Aliyekuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii na sasa ni Waziri wa Ulinzi na jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi (kushoto) akizungumza  na watendaji wa wizara hiyo (hawapo pichani) wakati wa makabidhiano ya ofisi  na aliyekuwa Naibu Waziri wake na sasa ameteulikuwa kushika nyadhifa ya Uwaziri Dkt. Seif Rashid (kulia), anayefuata ni Naibu Waziri wa  Wizara hiyo Dkt. Kebwe S. Kebwe.Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye ukumbi wa Waziri, wizarani hapo.TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI MOTOMOTO(USIPITWEEEE)
  DSC_1645Waziri wa  Afya na Ustawi wa jamii Dkt. Seif Rashid (kulia) akizungumza na watendaji wa wizara hiyo (hawapo pichani) na kutoa shukrani zake za dhati kwa aliyekuwa Waziri wake Dkt. Hussein Mwinyi  kwa ushirikiano wake kipindi alipokuwa akiongoza wizara hiyo. DSC_1660Naibu Waziri  Dkt. Kebwe S. Kebwe akizungumza na watendaji wa wizara hiyo na kuwataka kufanya kazi kwa ushirikiano na mahusiano mazuri  ili kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta hiyo DSC_1661Waziri wa Ulinzi Dkt. Mwinyi akiteta jambo na katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jami, Charles Pallangyo. DSC_1670Mawaziri hao wakisaini vitabu vya makabidhiano ya Muundo na Utekelezaji wa Wizara
DSC_1677 Aliyekuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Hussein Mwinyi  kushoto akimkabidhi kitabu hicho Waziri Mpya wa Wizara hiyo Dkt. Seif
DSC_1680 Naibu Waziri Dkt. Kebwe kulia, akikabidhiwa  kitabu na Waziri Dkt. Mwinyi
DSC_1693Mawaziri hao wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya makabidhiano pamoja na watendaji wa wizara hiyo. Wa kwanza kushopto waliokaa ni Katibu Mkuu, Charles Pallangyo, aliyekuwa Waziri wa afya na ustawi wa jamii Dkt. Mwinyi, Waziri mpya wa wizara hiyo Dkt. Seif nna wa mwisho kulia ni Naibu Waziri Dkt. Kebwe S. Kebwe ( Picha zote na Catherine Sungura-MOHSW)

No comments:

Post a Comment