Marehemu Ann Waithera
Mwili wa aliyekuwa mwandishi wa BBC aliyeaga dunia
wiki jana Ann Waithera umechomwa katika eneo la makaburi ya umma la
Lang'ata mjini Nairobi.
Lilikuwa ombi la Ann aliyekuwa anapenda sana
kutunza mazingira kuwa mwili wake uchomwe na kisha majivu yake yatupwe
kwenye mto na mengine kuwekwa katika eneo ambako kutapandwa mti kama
kumbukumbu kwake.Aliwahi kufanya kazi na mashirika mawili ya habari nchini Kenya, Nation na Citizen kama mtangazaji wa televisheni kabla ya kujiunga na shirika habari la kimataifa la BBC.
Katika BBC, alikuwa anafanya kazi kama ripota wa redio na televisheni hasa alipokwenda Ethiopia, kama ripota wa kwanza mwenye uwezo wa kuripoti katika lugha mbili, Kiswahili na Kiingereza.
Wakuu wa idhaa ya BBC Swahili David Okwemba, Ali Saleh na mkuu wa BBC Afrika Solomon Mugera wamemtaja Ann kama mchapa kazi na na mfanyakazi aliyependa kujituma na kwamba BBC imepoteza mwandishi habari mahiri sana Afrika
No comments:
Post a Comment