skip to main |
skip to sidebar
TAARIFA YA CCM KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MWENENDO WA EDWARD LOWASA
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEixAyxZCikW7WlOgLvsl2LAvLMTDTqyLf3UsmkEO_yxTwpu5RBbTqPSXHt2YNONWei2wXZ6bdI2ilGSwoqAxNAXkF6U-nhCGH1pdNzY_FodQuGhLOtcH3O6Ger0vNGmU5u7N7cjg-pbE8QC/s1600/ccm.jpg)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI --30/01/2014
Ndugu zangu waandishi wa habari, awali ya yote naomba niwasalimie na
niwapongeze kwa kufika -mwaka mpya 2014, pia naomba niwapongeze kwa kazi
kubwa ambayo mmekuwa mkiifanya hasa kuhakikisha watanzania wanapata
habari kwa kila jambo linaloendelea kila kona ya taifa letu la Tanzania.
Ndugu waandishi wa habari nimewaita hapa ili kuzungumza nanyi na
mnisaidie kufikisha ujumbe kwa watanzania hasa kuhusu jambo hili ambalo
limekuwa gumzo kwa watanzania wengi la mbio za urais 2015 kwa baadhi ya
watu ndani ya chama changu cha mapinduzi (CCM), kilichonisukuma zaidi na
kupata hamu ya kuongea nanyi ni baada ya kumsikia -na kumuona kijana
wetu ndani ya chama cha mapinduzi bwana Paul Makonda akiwa na ujasiri wa
kukemea vitendo mambo haya yanayofanywa na baadhio ya viongozi bila
uwoga wowote naomba tuchukue fursa hii kumpongeza sana kijana huyu.
Nadiriki kusema nampongeza kijana huyu hasa kwa kauli zake nzito na za
kijasiri kwa maslahi ya chama changu cha CCM ili chama kiendelee
kupendwa na kuchaguliwa na watanzania.
Pia itakuwa si busara kama sitawapongeza vijana wangu katibu mkuu wa
chama ndugu ABDULRAHMAN KINANA na NAPE NNAUYE kwa juhudi zao za dhati za
kujenga chama na kuendelea kuwaeleza wananchi juu ya misingi bora ya
chama cha mapinduzi (CCM) kwa kuwakemea viongozi wasiofaa bila kujali
cheo na umaarufu wao ndani ya chama na serikali, nawaomba waendelee -na
juhudi zao hizo nami naziunga mkono juhudi zao na kama kuna watru
wanaowabeza naomba wasijali kwani kukemea viongozi wasiofaa ndani ya
chama na serikali ni msingi wa chama chochote kilichounda serikali.
Aidha nawaomba watanzania wenzangu wazalendo wasikubali kukatishwa tama
na kikundi cha watu wachache wasio na mapenzi mema na taifa letu ambalo
limekuwa mfano wa kuigwa kwa amani, upendo, utulivu na mshikamano urithi
tulioachiwa na baba yetu wa taifa mwalimu julias kambarage nyerere
ndani na nje ya mipaka ya bara letu la afrika.
Ndugu zangu waandishi wa habari naomba niwaambie kuwa msemaji wa UVCCM
kijana wetu Paul Makonda namuunga mkono kwa -kitendo chake cha ujasiri
cha kumkemea ndugu EDWARD NGOYAI LOWASSA bila uwoga kwa jinsi
anavyokivuruga chama chetu kwa lengo la kutaka urais 2015 huku
secretariet ya chama ikiwa imekaa kimya wakati inajua kuwa muda wa
kuanza mbio hizi bado na kufanya hivi kwa sasa ni kukiuka misingi na
katiba -ya chama. Hapa najiuliza kuwa ile misingi imara ya uongozi ndani
ya chama chetu cha mapinduzi iko wapi? Mpaka tumuachie mototo ndio
akemee haya? Je, hapa chama kiko wapi?
Ukweli ni kwamba wanachama wetu na vijana wamekuwa njia panda huku
wakitamani kusikia tamko au karipio la chama juu ya suala hili la
harakati za urais 2015 bila mafanikio.
Naomba niseme kuwa bila kuwa na karipio au tamko la chama, hawa
wanaotumia pesa zao hadharani kwa lengo la kutafuta umaarufu na
ushawishi kwa vijana ili kupata madaraka wanaharibu misingi yetu bora ya
uongozi iliyowekwa na waasisi wetu ndani ya chama.
Kinachonisikitisha zaidi ni kuona juhudu za uongozi wa sasa wa chama
ngazi ya juu ikiwa ni pamoja na sekretarieti inayoongozwa na katibu mkuu
ABDULRAHMANI KINANA na katibu mwenezi NAPE NNAUYE za kutetea chama hiki
zinatiwa mchanga.
Ninaomba juhudi hizi zisibezwe na watu wenye nia njema na chama. Ukweli
ni kwamba vijana hawa wamekuwa na juhudi kubwa sana ya kujenga na
kuimarisha chama chetu -kwa wananchi kila pembe ya taifa letu kwa
kukemea na kueleza misingi ya uongozi bora. Swali: Je! Chama hakioni
haya mpaka vijana ndio waone?
Kwa hili ni lazima tubadilike ili kujenga chama chetu na naishauri
-secretariet ya chama lazima ichukue hatua mara moja, kijana huyu paul
makonda asingesema haya yote kama hana uhakika wa ushahidi wa wa haya
aliyoyasema na nampongeza sana.
Vijana na wanachama wengi wa CCM wamekuwa na hamu kwa muda mrefu ya
kutaka kujua msimamo wa chama chao bila mafanikio na ndio sababu ya
baadhi ya-wengine kupoteza mwelekeo.
Sisi tulikijenga chama hiki kwa taabu sana hapakuwa hata mtu mmoja
aliyediriki kutumia fedha zake kutaka madaraka. Nidhamu, busara na
uchungu wa rasilimali za taifa hili kwa maslahi ya wananchi ndio
vilituongoza kufuata misingi na maadili ya uongozi ndani ya chama na
serikali, ndio maana tunaumia sana kuona chama sasa kinataka kutekwa na
wenye fedha kwa uchu wa madaraka, mpaka tunashangaa na kujiuliza hizi
pesa wanatoa wapi? Na haya madaraka wanayotaka kwa kununua ni kwa
maslahi ya nani? Huku watanzania wakiendelea kuwa maskini.
Mfano hivi karibuni baadhi ya viongozi wa chama ngazi ya juu
wamejibishana kwenye vyombo vya habari,vitendo hivi havina tija kwa
chama na wala havileti umoja na mshikamano ambao umedumu ndani chama kwa
muda mrefu.
Mwisho Ninaomba sekretarieti ichukue hatua haraka kama alivyoomba kijana
wetu makonda na kweli kuchelewa kuchukua hatua jambo hili kumejionyesha
wazi kwamba utaleta kutokuelewana ndani ya chama kusiko kuwa na lazima.
JOHN SAMWELI MALECELA
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
No comments:
Post a Comment