![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgSYqO4E4MSvNlDHnuZoFL1-w9pD80FD0nfY6ylZRUf6C993brEpvYd6fuuM13zZc36vJhAObPBMgvYZ2k8yTItPgoDuBF0l6JFLPjElGfOfrxPLqooxAv8rl2s6piqSoDnD8cYPO23W6y4/s1600/unnamed+%2810%29.jpg)
Waziri wa
Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe(kushoto), akimtabulisha Katibu Mkuu wa
Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka(aliyevaa tai nyekundu) kwa
Waziri Mkuu wa Finland, Jyki Katainen, wakati Waziri Mkuu huyo
alipotembelea Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA), asubuhi
kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka hiyo.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEinejD9KAzlboaDLCt9AxR-bWQajKej07a6fPsPIVQFnnfj55wQAveGq6zvpBOUl3_731hTzRgKdDmPoMm1uL-KErGDI5dW_K-JhVH_IEhfnFpViBKnu8wFO10-HPrQ575R8hcYgFtRSnfC/s1600/unnamed+%2811%29.jpg)
Meneja wa
Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Awadh Massawe akitoa ufafanuzi wa namna
Bandari ya Dar es Salaam inavyofanya kazi kwa Waziri Mkuu wa Finland,
Jyki Katainen(wa tatu kutoka kushoto) , wakati alipotembelea Mamlaka
hiyo asubuhi kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka.
Kulia kwa Waziri Mkuu wa Finland ni Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison
Mwakyembe na kushoto kwa Waziri Mkuu huyo ni Waziri wa Niashati na
Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgPQy5JVBYoUUxhdCgnZjqpXmAiwxiZ4my0Wiz-1QBtqBaG4_n16Gno3gkyiP595nzX96I-ttqS-aKszUIjTi0EKA2JsCyG0uKxjH5AWYhuuwVGZ36FZdPHN3Dht-5_9nXkcZtndkDTI0El/s1600/unnamed+%2812%29.jpg)
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA),
Mhandisi Madeni Kipande, akitoa maelezo ya awali ya namna ambavyo
Bandari ya Dar es Salaam inavyofanya kazi kwa Waziri Mkuu wa Finland,
Jyki Katainen wakati alipotembelea Mamlaka hiyo asubuhi kuangalia
namna Mamlaka hiyo inavyofanya kazi. Aidha, Waziri Mkuu huyo alitembelea
Gati namba 1-7.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgPr2W2Ng4Xpt0QevfrN865AV-0o3Rw8YaIXElsE1zzZHyXyPXR6G9dbkgvg1rzkDfK8oHpnRbDqtFKYGnze41hfC6v9gVxBVN26nx5Cbz7a_UsyomXhzO9iI6zuLtRY3pjc9ysTmyCTUiV/s1600/unnamed+%2813%29.jpg)
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka akichangia mada wakati
wa Mkutano na Waziri Mkuu wa Finland, Jyki Katainen alipotembelea
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) asubuhi kuangalia
utendaji wa Mamlaka hiyo.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhqeRQTe0Hrwq3yeMDNq4FrjB-xtM5Ckscf_EM-R2mY6U_2C-uSXP6qJRUFKQKwf_KOb2cUzIOB0GtN5F9AeN2r6pmpPI2lJpKkpqb-2FYD1tVysaPgzWfMdgy6Vl4WSw1IEme3a_8VsI_L/s1600/unnamed+%2814%29.jpg)
Waziri wa
Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akimkabidhi zawadi Waziri Mkuu wa
Finland, Jyki Katainen wakati alipotembelea Mamlaka ya Usimamizi wa
Bandari Tanzania(TPA), kuangalia utendaji wa Mamlaka hiyo. Nyuma ya
Waziri Mwakyembe ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa
Bandari Tanzania (TPA).Picha na kitengo cha Mawasiliano
Serikalini-Uchukuzi.
No comments:
Post a Comment