Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unawatangazia
abiria wote na wananchi kwa jumla kuwa
kutokana na kujaa maji eneo kati ya
stesheni za Godegode na Gulwe mkoani Dodoma na kuharibu tuta la reli, unasikitika kutangaza kusitishwa kwa muda
huduma ya usafiri wa abiria kuanzia leo Ijumaa Januari 10, 2014 hadi
itakapotangazwa tena.
Wasafiri wote wenye tiketi halali wafike katika stesheni
walizokatia tiketi hizo kwa ajili ya kurejeshewa
fedha kuanzia leo!
Aidha taarifa hii
iwafikie wadau wote wa usafiri na huduma ya reli ya kati na kwamba uongozi wa
TRL unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza..
Imetolewa
na Ofisi ya Uhusiano kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Paschal
Mafikiri.
TRL Makao
Makuu,
Dar es
Salaam.
Januari 10,
2014
No comments:
Post a Comment