Mbunge
wa Jimbo la Chambani (CUF) Mhe. Yussuf Salim Hussein, akikabidhi
pikipiki mbili kwa Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad,
kwa ajili ya kuimarisha chama katika Wilaya za Kisarawe na Bagamoyo
Katibu
Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad, akikabidhi pikipiki mbili kwa
Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho (Bara), Julius Mtatiro, kwa ajili ya
kuimarisha chama katika Wilaya za Kisarawe na Bagamoyo. Pikipiki hizo
zimetolewa na Mbunge wa Chambani (CUF), Yussuf Salim Hussein. (picha na
Salmin Said, OMKR)
Na Hassan Hamad, OMKR
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad,
amewakumbusha viongozi wa majimbo kutekeleza ahadi wanazozitoa kwa
wananchi, ili kujijengea uaminifu katika maeneo yao.
Maalim
Seif ametoa kauli hiyo katika ofisi kuu ya CUF Buguruni, baada ya
kupokea pikipiki mbili kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Mhe.
Yussuf Salim Hussein (CUF), kwa ajili ya Wilaya za Kisarawe na Bagamoyo.
Amesema
kukabidhiwa kwa pikipiki hizo zenye thamani ya shilingi milioni tatu na
laki mbili, kunaonesha jinsi mbunge huyo anavyofuatilia na kutekeleza
ahadi zake kwa wananchi, na kutaka viongozi wengine waige mfano wa
mbunge huyo.
Mbunge
huyo wa Chambani amekabidhi pikipiki hizo kufuatia ahadi aliyoitoa kwa
wananchi wa Wilaya za Kisarawe na Bagamoyo, akiwa katika ziara ya Katibu
Mkuu wa Chama hicho mwezi uliopita.
Akizungumza
baada ya kukabidhi pikipiki hizo Mhe. Yussuf amesema ameamua kutekeleza
ahadi hiyo kwa muda mfupi, ili kujenga matumaini ya wanachama kwa
viongozi na chama chao.
Amesema
ataendelea kutekeleza ahadi alizozitoa kwa wananchi katika maeneo mbali
mbali, ili kuhakikisha kuwa chama hicho kinazidisha matumaini kwa
wanachama wake na wananchi kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment