Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) Jamali Malinzi, (katikati) akiongea na wandishi wa habari kuhusu Mpango Maalum wa Kuboresha timu ya Taifa, ‘Taifa Stars’ katika Ofisi za Shirikisho hilo zilizopo katikati ya jiji. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Selestine Mwesigwa na kulia ni Rais wa Chama cha Soka Zanzibar (ZDF), Ravia Idarous. |
SHIRIKISHO
la Soka Tanzania (TFF) limeanza mikakati ya kuiwezesha timu ya taifa ya
Tanzania ‘Taifa Stars’ kufuzu kwa Fainali za mataifa ya Afrika (AFCON)
mwakani baada ya kupanga timu hiyo kuweka kambi nchini Uholanzi.
Kambi
hiyo maalumu kwa timu hiyo itasaidia kujiandaa na hatua ya kufuzu
fainali hizo zitakazofanyika mwakani nchini Morocco na kushirikisha
jumla ya mataifa 16 yatakayofuzu.
Akizungumza
na jijini Dar es Salaam, Rais wa TFF, Jamal Malinzi amesema endapo
Stars itafanikiwa kupita katika hatua ya awali ya mchujo ikiwa itapangwa
kwenye hatua hiyo, wamepanga kuweka kambi nchini Uholanzi ili kujiandaa
na hatua ya pili ya makundi.
Malinzi
alisema wameamua kufanya hivyo ili kurudia historia ya mwaka 1979 ya
Stars kufuzu kwa mara ya mwisho michuano ya AFCON, iliyofanyika nchini
Nigeria, kwani Stars iliweka kambi Uholanzi kufanikiwa kufuzu kwa
fainali hizo.
“Tumepokea
barua ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) inayotueleza kuwa mechi zetu
za mchujo zitaanza kati ya mwezi Mei hadi Agosti kutokana na kiwango
chetu kuwa chini ya nchi 21 bora za bara hili, hivyo muda si mrefu
tunafikiria kurekebisha benchi lote la ufundi kwa pamoja na kuanza
mikakati ya timu hiyo.
“Huenda
timu yetu ikaanzia hatua ya mchujo kama CAF walivyotuandikia,
ikifanikiwa kufuzu katika hatua ya makundi ttumepanga kuweka kambi nje
ya nchi katika nchi ya Uholanzi, na huko timu itapata mafunzo ya kisasa
ili kufanya vizuri kwenye hatua ya makundi,” alisema Malinzi.
Pia
alisema wameshazungumza na Balozi wa Uholanzi hapa nchini kwa ajili ya
mipango yao hiyo, pia wamewataarifu wadhamini wakuu wa Stars, Kampuni ya
Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji cha Kilimanjaro Premier Lager ili
kuandaa bajeti ya ziara hiyo.
No comments:
Post a Comment