Heshima za mwisho: Kutoka kushoto, Victor Valdes, Carles Puyol, Xavi na Andres Iniesta wakiwa katika ibada ya kuuaga mwili wa Tito VilanovaSKWADI zima la Barcelona usiku wa jana limeuaga mwili wa aliyekuwa kocha wao, Tito Vilanova kabla ya mazishi yake.
Wachezaji wa kikosi cha kwanza walihudhuria ibada ya kuuaga mwili wa marehemu katika kanisa la Cathedral mjini Barcelona na kutoa heshima zao za mwisho kwa Vilanova, aliyefariki dunia Ijumaa akiwa na umri wa miaka 45 baada ya kusumbuliwa na maradhi saratani.
Mkewe na watoto wao wawili wa kike pia walihudhuria pamoja na mtoto wao kiume, Adria, anayechezea akademi ya Barca, na binti yake Carlota, alilia sana.
Dani Alves (kushoto) na Neymar kulia
Pumzika kwa amani: Tito Vilanova amefariki akiwa kijana wa miaka 45
"Leo tunamuaga mpendwa wetu,"alisema Bartomeu. "Nakuahidi, daima atadumu katika mioyo yetu na hatutamsahau milele,"aliongeza.
Kwaheri: Gerardo Martino (kushoto) na Rais wa Barca, Josep Maria Bartomeu pia walikuwepo
Waombolezaji mbalimbali wakiwa kanisani jana
Kipa wa Barca, Victor Valdes akiwasili na 'magongo' yake baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti aliloumia
No comments:
Post a Comment