Mwimbaji wa R&B, Chris Brown ameachiwa huru baada ya
kutumikia kukaa jela kwa siku 108 kati ya siku 131 alizokuwa amepangiwa na
mahakama hapo awali.
Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa mkali huyo wa ‘Loyal’
ameachiwa huru majira ya usiku wa manane kuamkia leo.
Awali mwimbaji huyo alihukumiwa kwenda jela kwa kipindi cha
mwaka mmoja lakini jaji alimpunguzia siku 116 alizokuwa amekaa rehab na siku 59
alizokaa rumande hivyo alitakiwa akae jela siku 131.
Chris Brown alihukumiwa kifungo hicho baada ya kuvunja
masharti ya kipindi cha matazamio (probation) aliyopewa kutokana na kesi ya
kumpiga Rihanna mwaka 2009.
Hata hivyo, bado yuko kwenye hatihati ya kurudi tena jela
kwa kuwa ana kesi ya kumshambulia mtu mmoja huko Washington DC ambayo
inatarajiwa kusikilizwa miezi michache ijayo.
Chris Brown amepost kwenye twitter ujumbe baada ya kutoka
jela.
No comments:
Post a Comment