Kamishina wa polisi kanda maalum ya Daresalaam Suleimani
Kova akitoa ufafanuzi jambo kwenye mkutano na waandishi wa Habari Jijin Dar es
Salaam,
JESHI la Polisi Kanda
Maalum Dar Es Salaam limefichua Siri ya kuongezeka Vitendo vya ujambazi katika maBenki mbalimbali hapa
nchini na kusema vitendo hivyo vinasababishwa na Wamiliki wa Mabenki hayo
kulipuuza
Jeshi la polisi,Kauli hiyo ya Jeshi la polisi Kanda ya Dar es Salaam
imekuja SIKU moja kupita baada ya watu
wanaosadikiwa kuwa ni Majambazi kuvamia katika Benki ya Stanbic tawi la
Kariakoo liloko mtaa wa Swahili na kukomba mamilioni ya pesa aliyokuwa nayo
Mteja,
Kauli hiyo
imetolewa Mda huu na Kamishna wa Polisi kanda Maalum Dar Es Salaam,Suleiman
Kova wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari Jijini Dar Es Salaam,ambapo
alisema watu wanaochangia Vitendo hivyo vya Ujambazi kuzidi kuongezeka katika
Mabenki mbalimbali hapa nchini ni Wamiliki wa Mabenki kupuuza ushauri wa Jeshi
la Polisi ,
Uliowataka
waache kutumia walinzi wa Makampuni Binafsi peke yake,watumia na Walinzi kutoka
Jeshi la polisi.
“Nataka
niwambie waandishi hivi vitendo vya Uvamizi kwenye mabenki viemtokana na wamiliki
wamabenki hayo kupuuza ushauri wetu uliowataka kwenyes shuhuri za Ulinzi kwenye
mabenki watumike Polisi tu,lakini wao wakapuuza,ukitaka kuamini Nenda kwenye
Mabenki yanayolindwa na Polisi kama utaona kama kunauvamini wowote
uonotokea,kwasababu majambazi hao wanashindwa kuvamia kutokana na umakini wa
Jeshi la Polisi”alisema Kova
Kamishna
Kova,alisema kwa sasa Jeshi la polisi limejipanga kuongea na Benki kuu(BOT)
ambaye ni kiongozi wa Benki zote hapa nchini na kutafuta ufumbuzi wa hili tatizo
la Mabenki Mengine kupuuza ushauri huo wa Jeshi la polisi.
Vilevile jeshi
hilo la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Limeeanza msako kali wa
kuwatafuta Majambazi watano waliovamia Jana kwenye Beki ya Stabinc Tawi la
Kariakoo lilioko mtaa wa Shwahili majira ya mchana.
Kwa Mujibu
wa Kamishna Kova alisema watu wa tatu kati yao waliingia ndani ya Benki hiyo
wakiwa na Mifuko Mikubwa wakijifanya ni wateja wanapeleka Fedha nyingi katika
Benki hiyo,watu hao walipoingia ndani walianza kuwalazimisha kuvuka wigo wa
wateja wa kwaida na kutaka kuingia kwa nguvu kupora Fedha.
Ambapo
Benki hiyo ya Stabinc ina mitambo ya Aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na Vingora
vya Tahadhari,ikasaidia kwa majambazi hao kushindwa kuingia ndani kuiba pesa za
Benki hiyo kutokana na Vingora hivyo kupiga kelele na kuanza kuwapa uwoga
majambazi hao ,ambapo walifanikiwa kuiba pesa za mteja mmoja ambae alikuwa
anataka kuweka pesa kwenye benki hiyo,
Kova
alisema Majambazi hao walipotoka nje ya Benki hiyo walipiga Risasi Juu ili
kuwapa Hofu wananchi walikuwa Nje ya Benki hiyo,ambapo kwa Mujibu wa Kamishna
Kova anasema bado wanaendelea kuwafuatilia majambazi hao.
Katika
Hatua nyingine Jeshi hilo la polisi Limejipanga ipasavyo kwenye sikuku ya IDD
El Haji 2014,ambapo jehi hilo limesema limepanga kushikirikiana na Vyombo
mbalimbali vya ulinzi na Usalama ikiwa ni pamoja na Kikosi cha Zima Moto na Uokoaji,Kampuni Binafsi za
ulinzi lengo ni kuhakikisha wananchi wanafurahia kwa utulivu na amani kwenye
sikuku hii.
No comments:
Post a Comment