KLABU
ya Yanga imembwaga mshambuliaji wake Mganda, Khamis Kiiza ‘Diego wa
Kampala’ baada ya kusajiliwa kwa Wabrazil wawili, Andrey Coutinho na
Geilson Santos Santana `Jaja`.Baada
ya Jaja kusaini mkataba wa miaka miwili jana makao makuu ya klabu ya
Yanga, kulikuwa na utata ni mchezaji gani atapigwa chini kati ya Kiiza
na Emmanuel Anord Okwi.Awali ujio wa Jaja ulielezwa kuwaweka kitimoto Kiiza na Okwi, huku mmojawapo akitakiwa kutolewa kafara.
Taarifa
za uhakika ambazo mtandao huu umezipata ni kwamba kocha Maximo
amependekeza kuachwa kwa Kiiza kutokana na ripoti iliyoachwa na Hans Van
Der Pluijm.
Mzigo
huo uliofuatwa chini ya kapeti unasema kuwa Pluijm katika ripoti yake
aliyowasilisha kwa viongozi baada ya kumalizika kwa msimu uliopita,
alisema ili Emmanuel Okwi acheze Yanga sc, lazima Kiiza aondolewe.
Kwa kuzingatia mapendekezo hayo, Maximo amefuata ushauri huo na sasa Kiiza rasmi anaondoka Jangwani.
Katika
hatua nyingine, imeelezwa na chanzo cha uhakika kuwa Maximo amewabana
viongozi wa Yanga akiwataka wajenge uwanja wa mazoezi wa Kaunda ili
kuepukana na adhaa anayoipata.
Maximo amewakazia na amesema hakuna jinsi, lazima uwanja huo ujengwe muda huu.
Pia amewataka viongozi kuboresha vyumba vya jengo la Jangwani ili wachezaji wote waishe pale.
Taarifa zinasema, Maximo amesema haiwezekani timu kukaa saa mbili kwenye foleni inapoelekea uwanjani na kurudi kambini.
Kwa
mazingira hayo anataka wachezaji wake wakae makao makuu ya Yanga, mitaa
ya Twiga na Jangwani, halafu uwanja wa Kaunda ujengwe.
Mbrazil, Marcio Maximo anafahamika kwa kuwa na msimamo mkali katika mambo yake.
No comments:
Post a Comment