Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za kampuni hiyo zilizoko Moroco jijini Dar es salaam wakati akielezea kuhusu kukamilika kwa maadalizi ya uzinduzi wa albam ya mwimbaji wa muziki wa injili Rose Muhando inayojulikana kama "Kamata Pindo la Yesu" maarufu FACEBOOK utakaofanyika kwenye ukumbi wa VIP Diamond Jubilee Agosti 3/ 2014 jijini Dar es salaam na kufuatiwa na maonesho mengine katika mikoa ya Tabora, Geita na Mwanza mara baada ya uzinduzi wa Dar es salaam, Msama ameongeza kuwa waimbaji mbalimbali wa muziki wa injili wamethibitisha kushiriki katika uzinduzi huo ambao ni
John Lisu, Upendo Kilahiro, Upendo Nkone , Ephraim Sekereti na wengine wengi, Tiketi zinapatikana katika vituo vifuatavyo Maduka yote ya Msama Promotion Kariakoo na Posta, Bestbite Namanga, vituo vya mafuta Puma Mwenge na Airport. Watu wote mnahimizwa kuwahi kununua tiketi ili kujihakikishia nafasi katika uzinduzi huo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu baadhi ya mapato yatakayopatikana kuelekezwa kwenye vituo vya watoto yatima.
Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akifafanua jambo kuhusu tikaeti ambapo amesema zinapatikana katika vituo vya kuuzia tiketi ambayo ni Maduka yote ya Msama Promotion Kariakoo na Posta, Bestbite Namanga, vituo vya mafuta Puma Mwenge na Airport watu wote mnahimizwa kuwahi kununua tiketi ili kujihakikishia nafasi yake katika uzinduzi huo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mazungumza ya Mkurugenzi ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion wakati akielezea mambo mbalimbali kuhusu uzinduzi wa Albam ya Shikilia Pino la Yesu ya mwimbaji Rose Muhando.
No comments:
Post a Comment