Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, akikata
utepe kuzindua rasmi Msikiti wa ‘Masjidil Huda’ uliojengwa na mfanyabiashara
maarufu nchini, Said Salim Bakhresa
katika eneo la Uwanja wa Chamazi, Mbagala jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Mwenyekiti huyo wa Makampuni ya SSB, Said Salim
Bakhresa, ambapo pia uzinduzi huo uliofanyika leo Julai 4, 2014, ulihudhuriwa
na baadhi ya Viongozi wa Kiserikali akiwemo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mke wa Rais, Mama Salma
Kikwete, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na wengineo. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal (wa tatu kulia) Rais Mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan
Mwinyi (wa pili kushoto) Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana ( wa pili kuli)
Mwenyekiti wa Makampuni ya SSB, Said Salim Bakhresa (katikati) na Sheikh Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (kushoto) wakijumuika na waumini wa
dini ya Kiislam, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mkititi wa ‘Masjidil Huda’ na
Swala ya Ijumaa uliofanyika leo Julai 4, 2014, Chamaz jijini Dar es Salaam.
Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na wenyeji wake wakati alipowasili Msikiti
wa ‘Masjidil Huda’ uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuhudhuria
uzinduzi wa msikiti huo uliofanyika leo Julai 4, 2014. Picha na OMR
No comments:
Post a Comment