Pages

Friday, July 4, 2014

RAIS MSTAAFU ALI HASSAN MWINYI AZINDUA MSIKITI WA MASJIDIL HUDA CHAMAZI MBAGALA JIJINI DAR LEO


Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, akikata utepe kuzindua rasmi Msikiti wa ‘Masjidil Huda’ uliojengwa na mfanyabiashara maarufu nchini, Said Salim Bakhresa  katika eneo la Uwanja wa Chamazi, Mbagala jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Mwenyekiti huyo wa Makampuni ya SSB, Said Salim Bakhresa, ambapo pia uzinduzi huo uliofanyika leo Julai 4, 2014, ulihudhuriwa na baadhi ya Viongozi wa Kiserikali akiwemo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na wengineo. Picha na OMR


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (wa tatu kulia) Rais Mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi (wa pili kushoto) Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana ( wa pili kuli) Mwenyekiti wa Makampuni ya SSB, Said Salim Bakhresa (katikati) na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (kushoto) wakijumuika na waumini wa dini ya Kiislam, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mkititi wa ‘Masjidil Huda’ na Swala ya Ijumaa uliofanyika leo Julai 4, 2014, Chamaz jijini Dar es Salaam. Picha na OMR



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na wenyeji wake wakati alipowasili Msikiti wa ‘Masjidil Huda’ uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuhudhuria uzinduzi wa msikiti huo uliofanyika leo Julai 4, 2014. Picha na OMR

No comments:

Post a Comment