Shambulio katika kambi ya jeshi ya kikosi cha kumlinda rais
wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo limezuiwa, kwa mujibu wa maafisa wa
serikali.
Hali imerejea kuwa ya utulivu na kundi dogo la
"waliojipenyeza" limezidiwa nguvu, imesema serikali ya Kinshasa.
Milio mizito ya bunduki ilisikika katika
kambi ya Tshatshi,
kwa karibu dakika 30.
Mamlaka hazijasema nani amehusika na shambulio hilo.
Wakazi wa eneo hilo walihamishwa, na uwanja wa ndege wa
kimataifa kufungwa.
Mlinzi mmoja wa kikosi cha rais ameliambia shirika la habari
la AFP kuwa watu 20 waliokuwa na mavazi ya kiraia wamezidiwa nguvu.
Mwanajeshi mwingine ameliambia shirika la habari la Reuters
kuwa washambuliaji wanne wameuawa.
Shambulio katika kambi ya Tshatshi mwezi Disemba mwaka jana
pia lilidhibitiwa.
No comments:
Post a Comment