Vitalii Sediuk aliondolewa katika
sehemu hiyo na polisi waliomfunga pingu
Mwanamume mmoja amekamatwa baada ya
kumshambulia kwa makonde muigizaji maarufu duniani Brad Pitt usoni mwake katika
sherehe ya ufunguzi wa filamu ya Maleficent mjini Los Angeles.Mwandishi habari
wa Ukraine Vitalii Sediuk - anayejulikana kwa kuwahahadaa watu mashuhuri
duniani ,aliripotiwa kuonekana akivuka kizuizi na kumkumbatia Brad kabla ya
kumpiga usoni.Kijana huyo mwenye umri wa miaka 25 kwa jina Vitalii Sediuk,
alikamatwa na walinzi wa Brad baada ya kupambana naye na kukabidhiwa kwa polisi
waliokuwa wanshika doria.
Sediuk aliondolewa na polisi katika
tamasha la filamu la Canes wiki jana baada ya kuingia bila idhini.Pitt alikuwa
anakutana na mashabiki wake kabla ya kushambuliwa ingawa hakujeruhiwa vibaya.Inaaminika
kuwa Pitt alipigwa usoni ingawa polisi wanachunguza kisa hicho
Pitt na mkewe Angelina Joli ndio
waigizaji nyota katika filamu hiyo mpya ya Maleficent ambayo ilikuwa
inazinduliwa na kampuni ya Disney.Msemaji wa kampuni ya Disney iliyotengeza
filamu hiyo alisema kuwa walisikitishwa na kitendo hicho na kwamba polisi
wanafanya uchunguzi.
Sediuk alizuiliwa na polisi Jumatano
usiku akisubiri kuachiliwa kwa dhamana ya dola 20,000.Polisi walisema kitendo
cha kijana huyo kilikuwa cha maksudi ingawa uchunguzi bado utafanywa.
No comments:
Post a Comment