Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, August 22, 2014

HIZI NDIO SABABU ZA BOB JUNIOR KUBADILISHA JINA LA STUDIO YAKE

Studio ya Bob Junior imebadilika kutoka ‘Sharobaro Records’ na kuwa ‘Sharobaro Music’.
Bob Junior ameiambia Blog hii kuwa sababu za kubadilisha jina hilo ni kutokana na kubadilika kwa muziki atakaokuwa akiutengeneza kama mtayarishaji wa muziki na pia kutokana na kununua vifaa vipya.


“Ilikuwa ni mahesabu ya kwangu mimi na kampuni yangu, tulikuwa tunataka kuibadilisha kuanzia muziki, sound kwasababu kuna vyombo vipya ambavyo vimekuja kutoka Marekani na pia nilikuwa nimetengeneza sound mpya siku nyingi,” amesema.

Mtayarishaji huyo wa muziki amedai kuwa uamuzi huo umekuja ili kuwathibitishia watu kuwa anaweza kufanya muziki wa aina mbalimbali.CHANZO Kikwetu Blog

No comments:

Post a Comment