Malaysia iko katika siku ya maombolezi ya kitaifa baada ya
kupokea miili 20 ya wahanga wa mkasa wa ndege ya Malaysia MH17 iliyotunguliwa
Ukraine mwezi uliopita.
Miili ilipokelewa na kupewa heshima za kitaifa.
Majeneza yalikuwa yamefunikwa na bendera za taifa na
ilibebwa na wanajeshi kabla ya kusafirishwa kwa magari ya kubeba maiti
iliyozipitishwa karibu na
mfalme na waziri mkuu kabla ya kukabidhiwa kwa
familia husika.
MH17 iliangushwa katika eneo la waasi Mashariki ya Ukraine
mwezi uliopita.
Machi mwaka huu ndege nyingine ya Malaysia ilitoweka katika
bahari hindi na mwandishi wa BBC amesema kuwa shirika hilo la ndege linaendelea
kutatizwa na matukio hayo mawili.
Maombolezi Kuala Lumpur
Wasafiri wote 298 waliokuwa katika ndege hiyo ya MH17
walifariki 43 kati yao wakiwa raiya wa Malaysia.
Ndege iliyobeba miili hiyo ilikuwa imetengwa kwaajili ya
shughuli hiyo kutoka Amsterdam na kutua saa nne saa za huko.
Bendera ya taifa itapepea nusu mlingoti kote nchini na
dakika moja ya kimya itazingatiwa.
Kikundi kidogo cha wanajeshi wa Malaysia kilienda hadi
karibu na ndege hiyo kulinda majeneza hayo yalipokuwa yakitolewa kwa ndege huku
magari makubwa meupe ya mazishi yakiwa yamepangwa kuzipokea miili hiyo.
Majeneza yote yamefunikwa kwa bendera ya taifa na miili
mitatu ya hiyo 20 imechomwa nchini Uholanzi.
Baadhi ya Miili 20 ya wahanga wa ndege ya Malaysia MH17
imezikwa Kuala Lumpur
New Straits Times ilisema sekta ya uchukuzi ya umma nchini
humo ikiwemo ile ya reli ya taifa na reli moja ya Kuala lumpur zitasimamisha
shughuli zao kuzingatia dakika mbili za kimya kwa heshima ya wahanga wa mkasa
huo.
Vibanda maalum kwenye barabara kuu vitakuwa na ishara za
kielektroniki kuwaeleza madereva washuke kutoka kwa magari yao ilikutoa
heshima.
Msemaji wa ndege za Malaysia alisema kwamba kampuni hiyo
ingepanga kipindi cha maombi ambacho kingefanywa wazi kwa mtu yeyote ili kutoa
maombi na heshima zao kwa walioaga.
Akiongeza alisema kwamba kampuni hiyo ya ndege za Malaysia
imehuzunishwa sana na tukio hilo la kuogofya .
Aidha imekuwa muda mrefu wa kungoja kwa familia na marafiki
wa wasafiri na wafanyakazi waliokuwa katika ndege MH17
No comments:
Post a Comment