Alisema mtuhumiwa huyo aliweka dawa hizo kwenye pakiti na kuziuza sehemu mbalimbali kwa Sh1,000.
“Tulimkamata Agosti 2 mwaka huu katika mtego maalumu uliowekwa na askari wa upelelezi,” alisema Kova.
Alisema uchunguzi wa awali ulibaini kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa akitumia mbinu hiyo kwa muda mrefu kabla ya kukamatwa.
Kova alisema dawa alizokuwa akiuza mtuhumiwa ni zile za viwandani kama cocaine, heroine na bangi.
Wakati huohuo, polisi wanamshikilia askari polisi aliyerusha bomu la machozi, Mbagala Zakhiem na kumjeruhi mkazi mmoja wakati wakimsaka mtuhumiwa wa wizi wa pikipiki.
Aliyepigwa na bomu hilo ni Mwanaharusi Hamis ambaye amelazimika kukatwa kiganja cha mkono wa kulia baada ya kujeruhiwa vibaya.
Mwanaharusi alilipuliwa na bomu hilo Agosti Mosi mwaka huu, saa 3 usiku akiwa nyumbani kwake na sasa amelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
CHANZO::mwananchi
No comments:
Post a Comment