Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, September 18, 2014

AMIRI JESHI MKUU WA JESHI LA TANZANIA DR. JK AWAPANDISHA VYEO WANAJESHI 7 MAJINA YAO HAYA HAPA




Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe Jakaya Mrisho Kikwete, kwa mujibu wa Kanuni za Majeshi ya Ulinzi, Ayaya 7.01 Kifungu cha (3) amewapandisha cheo Maafisa Saba (7) kutoka Brigedia Jenerali kuwa Meja Jenerali kuanzia Septemba 12, 2014. Waliopandishwa cheo ni kama ifuatavyo:-


1. Brigedia Jenerali Gaudence Milanzi kuwa Meja Jenerali.
2. Brigedia Jenerali James Mwakibolwa kuwa Meja Jenerali.
3. Brigedia Jenerali Ndetaulwa Zakayo kuwa Meja Jenerali.
4. Brigedia Jenerali Venance Mabeyo kuwa Meja Jenerali.
5. Brigedia Jenerali Simon Mumwi kuwa Meja Jenerali.
6. Brigedia Jenerali Issa Nassor kuwa Meja Jenerali.
7. Brigedia Jenerali Rogastian Laswai kuwa Meja Jenerali.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange amewavisha cheo cha Meja Jenerali kwa niaba ya Rais. Sherehe hizo fupi zitafanyika Makao Makuu ya Jeshi Upanga Dar es Salaam.

Aidha, Meja Jenerali Milanzi, ameteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa (NDC) kufuatia nafasi iliyoachwa na aliye kuwa Mkuu wa Chuo hicho Luteni Jenerali Charles Makakala ambaye amestaafu.

Taarifa imetolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano
Makao Makuu ya Jeshi

Dar es salaam

No comments:

Post a Comment