Kava la Filamu ya KITENDAWILI iliyochezwa na Single Mtambalike au Rich Rich, Irene Veda na Haji Adam ambayo inasambazwa na Kampuni ya Proin Promotions Limited
Filamu zilizochaguliwa kuingia katika Tamasha hizo kutoka kampuni mahiri ya utengenezaji na usambazaji wa filamu Tanzania ya Proin Promotions Limited na ambazo zina ubora wa kimataifa huku filamu hizo kutoka Proin Promotions ltd zikiiwakilisha vyema Tanzania.
Filamu zilizoingia katika tamasha hilo na zenye ubora wa Kimataifa kutoka Kampuni ya Proin Promotions Ltd ni pamoja na Kitendawili(feature), Kigodoro(Feature), Sunshine(Feature), Network(Feature).
Filamu hizi za Kitanzania zina sehemu moja tu yaani part 1 na sio Part 1 na part 2. Kwa kuzingatia vigezo vya kimataifa vya filamu kuwa Na Sehemu Moja tu yaani Part 1 ndio sababu filamu kutoka Proin Promotions zimefanikiwa kupita mchujo ambapo Kampuni ya Proin Promotions Ltd ambayo haitaki part 1 na part 2 kwa lengo la kukuza tasnia ya filamu nchini.
Filamu za Tanzania zenye part 1 na part 2 zimetupwa nje sababu waandaji na wataalamu wa nje wameziona hazina ubora wa muda katika standard ya kimataifa na vigezo vinginevyo.
Filamu hizo za Tanzania zitaonyeshwa pamoja na filamu mbalimbali nyingine zilizopita katika mchujo huo toka mataifa mabalimbali ikiwemo Canada, Kenya, Uganda, Austalia, Rwanda, Spain, S.Africa, Guinea Bisau, Brazil, Nigeria, Switzerland, Argentina, UK, Burundi, Morocco. Ili kuona List nzima ya filamu hizo ingia hapa Selected Films Arusha Film Festival 2014.
Vilevile kutakuwa na zoezi la utoaji wa tuzo katika tamasha hilo la filamu kwa kazi nzuri.
No comments:
Post a Comment