Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya
jinai kamishina wa polisi Isaya Mngulu akizungumza na waandishi wa habari leo mjini mjini Songea mkoani Ruvuma
---------------------
Na Nathan Mtega wa demasho.com,Songea
JESHI la polisi chini limethibitisha kuwa kitu kilichokuwa
kinadaiwa kuwa nio bomu lililorushwa mjini Songea mkoani Ruvum Septemba 16
mwaka huu majira ya saa 1.25 usiku katika eneo la Misufini na kuwajeruhi askari
polisi watatu kati ya wanne waliokuwa doria kuwa ni bomu la kutupwa kwa mkono
lililotengenezwa kienyeji.
Akitoa taarifa ya uchunguzi
wa tukio hilo kwa waandishi wa habari mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya
jinai kamishina wa polisi Isaya Mngulu amesema bomu hilo lilirushwa na watu
wasiojulikana na kuwajeruhi askari polisi watatu waliokuwa doria siku hiyo wa
kituo kikuu cha polisi cha mjini Songea ambao ni G.5515 PC John,G7351 PC
Ramadhan na WP 10399 Felista ambao baaada ya kujeruhi kwa bomu hilo walikibizwa
katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma iliyopo mjini Songea kwa matibabu.
Amesema askari PC John aliyepata majeraha kiasi alipatiwa
matibabu siku hiyo na kuruhusiwa huku askari wawili PC Ramadhan na WP Felista wakiendelea
kupatiwa matibabu hospitalini hapo na hali zao zinaendelea vizuri.
Aidha amesema jeshi las polisi makao makuu kwa kushirikiana
na jeshi la polisi mkoani Ruvuma na vyombo mbali mbali vya ulinzi na usalama
vinaendelea na uchunguzi zaidi ikiwa ni pamoja na kutafuta taarifa za
waliohusika na tukio hilo ambalo mpaka sasa hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana
nalo.
Amesema jeshi la polisi linaamini kuwa wahusika waliofanya
tukio hilo ni sehemu ya jamii inayoishi mjini Songea au yenye mahusiano na
wenyeji wa Songea na mtu aliyetengeneza bomu hilo lazima kuwa kuna mtu au watu walioshuhudia au wanaomjua kwa
maana kwamba hakuwa pekee yake na ni imani ya jeshi la polisi kuwa kuna baadhi
ya wananchi wanaweza kuwa wanawafahamu wahusika wa tukio hilo wasisite
kushirikiana na jeshi la polisi kuwafichua ili kuendeleza ushirikiano mwema na
jeshi la polisi kwa ulinzi.
Katika hatua nyingine mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya
jinai Kamishina wa polisi Isaya Mngulu ametoa wito kwa wananchi kuendeleza
ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na timu ya upelelezi kutoka
makao makuu ya jeshi la polisi kwa ajili ya kuwapata wahusika wa tukio hilo ambalo
limetokea kwa mara ya kwanza mkoani Ruvuma na lisipofanyiwa kazi ipasavyo
linaweza kutoa mwanya kwa wahalifu wa aina hiyo kuendeleza uhalifu huo kwa
wananchi pamoja na jeshi la polisi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment