Per Mertesacker, Miroslav Klose na Philipp Lahm baada ya
kukabidhiwa tuzo zao Esprit Arena
WAKONGWE Miroslav Klose, Philipp Lahm na Per Mertesacker
wamepewa tuzo za heshima usiku huu kabla ya mchezo wa kirafiki kati ya
Ujerumani na
Argentina Uwanja wa Esprit Arena.Watatu hao waliichezea Ujerumani
katika fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2014 dhidi ya Argentina kabla ya kuamua
kustaafu soka ya kimataifa.
Klose, ambaye ni mfungaji bora wa kihistoria wa Ujerumani
kwa mabao yake 71, ametungika daluga baada ya kuwa mfungaji wa mabao mengi
zaidi katika historia ya Kombe la Dunia.
MCHANGO WAO KATIKA TIMU YA TAIFA UJERUMANI...
Miroslav Klose (Lazio) - Mechi 137, mabao 71
Philipp Lahm (Bayern Munich) - Mechi 113, mabao 5
Per Mertesacker (Arsenal) - Mechi 104, mabao 4
No comments:
Post a Comment