Mtoto Happiness Rioba(10) aliyedaiwa kuzamia kwenye ndege
kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar bila kugundulika, ametoweka tena nyumbani
kwao baada ya kukutanishwa na mama yake mzazi Sara Zefhania.
Happiness ambaye ni mkazi wa eneo la Mkokozi, Wilaya ya
Mkuranga mkoani Pwani inadaiwa
ametoweka katika mazingira ya kutatanisha.
Akizungumza na Mwananchi jana, Sara alisema mwanawe
alitoweka jana saa sita mchana na kutokomea kusikojulikana.
Alisema asubuhi mtoto wake aliamka salama bila tatizo lolote
na muda wote walikuwa pamoja kwa kuwa alikuwa na wageni kutoka kituo cha
televisheni cha ITV, waliomuahadi kumtembelea nyumbani kwa lengo la kumuona
Happiness.
“Aliamka vizuri tu na muda wote alikuwapo nyumbani, lakini
ilipofika saa sita mchana, nilipigiwa simu na waandishi wa habari wa ITV kuwa
nikawachukue katika kituo cha daladala... kabla sijaondoka nilimwambia mwanangu
nakwenda kupokea wageni, lakini niporejea nyumbani na wageni hatukumkuta,”
alisema Sara.
Alisema baada ya kumkosa alianza kumtafuta akishirikiana na
waandishi hao pamoja na majirani, lakini hawakufanikiwa kumpata ndipo alipotoa
taarifa kwa mjumbe wa Serikali za Mitaa na kuwataarifu ndugu, jamaa na
marafiki.
Aidha, aliongeza mwanawe alipokuwa Zanzibar alifanya mambo
ya ajabu likiwamo kuongea na paka, kula chakula kwa kutumia mkono wa kushoto,
kutokuongea na watu pamoja na kutoweka katika mazingira ya kutatanisha.
No comments:
Post a Comment