Mwanamke wa Mexicana, Leandra Becerra mwenye umri wa miaka
127 anaetajwa kuwa mtu mwenye umri mkubwa zaidi duniani ameeleza siri ya kuishi
miaka mingi zaidi.
Kwa mujibu wa mjukuu wake mwenye umri wa miaka 45, bibi huyo
alimueleza kuwa siri ya ‘yeye’ kuishi miaka mingi ni kula vizuri, kulala kwa
muda mrefu na kuishi bila kuolewa. Bi Leandra ambaye
alizaliwa August 31, 1887
alikuwa mpiganaji wakati wa mapinduzi ya Mexico mwaka 1910-1919 na alikuwa
kiongozi wa kundi la ‘Adelitas’ ambalo lilikuwa linaundwa na wanawake wanaoenda
vitani na waume zao.
Bibi huyo ambaye ana wajukuu wengi huku mjukuu wake mkubwa
akiwa na umri wa miaka 73, tayari ameshawazika watoto wake watano.
Mjukuu wake aliiambia gazeti la El Hozizonte la Mexico kuwa
bibi huyo hivi sasa anatatizo la kubwa la kusikia.
Ameeleza kuwa bibi huyo mara nyingine hulala mfululizo kwa
muda wa siku tatu huku akipewa chakula pale anaposhituka. Lakini akiamka
hupenda kula mlo kamili kwa uhakika, kuimba, kutaniana na kusimulia hadithi
mbalimbali zinazohusu maisha na mapambano ya mapinduzi ya Mexico.
CHANZO:BONGO5
No comments:
Post a Comment