1.Kutaka kujua inauzuri gani kuwa na
mwanamke mwingine nje ya huyu aliyenae. Kama ana mpenzi mnene basi anataka tu kujua wanawake wembamba
wakoje?
2.Jamii Yetu Kuhisi ni Ruksa kwa mwanaume
kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja kutokana na tamaduni mbovu tulizorithi kutoka kwa
mababu zetu. Mwanaume anaweza asiwe na tamaa ya kuwa na mpenzi mwingine lakini
tu kwa kuona ataonekanaje kwenye jamii anaamua kuwa na mpenzi mwingine.
3. Wanaume wengi hatujui kusema hapana; Ikitokea msichana
amekushawishi basi wengi huona hili kama bahati yaani kawaacha wanaume wangapi
mpaka kanifuata mimi! Kumbe unajiangamiza.
4 Marafiki wanaomzunguka; Wengi wa
wanaume hujikuta wamekuwa na wapenzi wan
je kutokana tu na mrafiki anaokaa nao kuwa na tabia hii mbaya! Hivyo humbidi
awe na tabia hiyo ili awe sehemu ya kundi hilo.
5. Kudhihirisha UWANAUME wake; Pengine ni
kwa imani potofu, marafiki, au tu kwa kumkomoa mpenzi wake, wanaume wengi
huamua ku “cheat” kuonyesha tu yeye ni mwanaume wa shoka, na anaweza kufanya
lolote, yaani yeye sio “jinsia-mbili”.
6. Kutimiza Mahitaji yake anayoyakosa kwa
mpenzi aliyenae hivyo kutafuta sehemu nyingine anayoona atapata.
7. Familia yake ni watu wa namna hiyo hii
ni hatari; Kuna wanaume ambao ni wazinzi kwa kuwa tu baba yake, kaka zake, na
watu aliolelewa nao wana tabia hii. Ni ngumu sana kumbadili mwanaume huyu.
8. Pombe, na madawa ya Kulevya
9. Kumzoeza vibaya kwa maneno kama “Wewe
iba tu lakini usikamatwe” Anahisi huwezi kumfanya chochote na utaizoea tabia
yake hiyo
10. Kutaka kuona kama bado ana “uwezo” hasa
kwa wanaume wenye Umri wa zaidi ya miaka 40.
MAKALA HII NA KUMI MUHIMU
MAKALA HII NA KUMI MUHIMU
No comments:
Post a Comment