Aliyekuwa waziri wa mambo ya nje Burkina Faso Michel
Kafando, ametajwa kuwa rais wa mpito nchini humo.
Jitihada zimekuwa zikiendelea nchini humo kumchagua kiongozi
wa mpito kufuatia kuidhinishwa hapo jana na jeshi na viongozi wa mashirika ya
kiraia kwa mpango wa mwaka mzima utakaohakikisha kufanyika uchaguzi.
Kafando alikuwa mmoja kati ya watu wanne ambao wangechukua
wadhifa huo, wakiwemo waandishi
wawili na msomi mmoja.
Viongozi wa mashirika ya kiraia na wawakilishi wa jeshi
walishughulika hadi usiku katika mji wa Ouagadougou kuamua nani atachukua
wadhifa huo wa rais wa mpito.
Kwa mujibu wa makubaliano hayo ya mpito, ilikuwa ni lazima
awe raia ambaye hatogombea katika uchaguzi huo.
Mwishowe walimchagua raia aliyependwa zaidi na jeshi, mwenye
umri wa miaka 72 na waziri wa mambo ya nje wa zamani Michel Kafando, Sasa ni
lazima amchague waziri mkuu ambaye anaweza kuwa raia au afisa wa jeshi kuongoza
serikali ya watu 25 ya mpito.
No comments:
Post a Comment