Wanawake wawili wamekufa wakati tope zito lilipovunja nyumba
karibu na mji wa Lugano nchini Uswisi.
Katika mpaka, mstaafu na mjukuu wake wa kike waliuawa wakati
maporomoko ya udongo yalipoifukia nyumba yao.
Mvua kubwa inatarajiwa kuendelea katika eneo hilo, na nchi zote mbili zimetoa ilani ya tahadhari.
Viwango vya maji katika maziwa Lugano na Maggiore, ambavyo vilionekana kuwa chini ,sasa viko juu kabisa na kutishia usalama.
Makazi na maeneo ya biashara, kama vile shamba karibu na ziwa Maggiore nchini Italia, yamekatwa mawasiliano kutokana na mafuriko.
Eneo hilo limepata mvua zaidi katika siku chache kuliko ilivyotarajiwa kawaida katika mwaka.
Kingo za mto Ticino zimevunjika karibu na Vigevano kaskazini mwa Italia.
Kaskazini zaidi, katika mkoa wa Ticino nchini Uswisi, wafanyakazi wa uokoaji walikuwa wakiwatafuta watu walionusurika Jumapili baada ya matope kuporomoa kilima na kuharibu jengo.
Serikali ya Uswisi imesema wanawake wawili wenye umri wa miaka 34 na 38 walipoteza maisha wakati maporomoko ya udongo yalipokumba jengo moja katika kijiji cha Davesco-Soragno.
No comments:
Post a Comment