Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamanda
wa Kanda hiyo, Kamishna (CP), Suleiman Kova, alisema majambazi hao
wamekamatwa katika oparesheni maalumu iliyoanza rasmi Oktoba 28 mwaka
huu hadi sasa.
Kamanda Kova, aliwataja majambazi hao kuwa ni
Ramadhani Said (37), mfanyabiashara wa mitumba mkazi wa Temeke, Rajab Ally (39), mfanyabiashara mkazi wa Mbagala, Dash John (38), mkazi wa Mbagala Chamazi na Shabani Said (28), dereva wa bodaboda mkazi wa Pugu Kajiungeni ambaye amekamatwa na silaha ya S/Gun Pump Action iliyofutwa namba yenye risasi.

Wengine ni Mohamed Mondo (32), mkazi wa Sinza Legho, Hamid Ramadhan
(25), mkazi wa Mburahati, Carlos Kisitu (28), mkazi wa Mbagala Chamazi,
Selemani Shabani (31), dalali wa nyumba mkazi wa Mwananyamala Kisiwani.
Aliwataja waliouwawa ni Salum Kombo (27), dereva wa bodaboda, Mkazi
wa Temeke, ambaye alikuwa silaha aina ya SMG NO. 789317 pamoja na risasi
12 na Mathias Emmanuel ambaye alikutwa na bastola iliyofutwa namba
ikiwa na risasi mbili ndani ya magazine.
“Jambazi huyu alikuwa anatafutwa muda mrefu kwa kujihusisha na
matukio ya aina mbalimbali ya unyang’anyi wa kutumia silaha likiwemo
tukio la kukatwa mkono askari Polisi eneo la Pugu Mnadani na kisha
kupora silaha aina ya SMG,” alisema Kova
- Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment