Polisi mjini Mombasa Pwani ya Kenya wanasema wamepata silaha
nyingine zaidi ikiwemo mabomu katika msikiti wa tatu ambao ulifanyiwa msako
Msako huo katika msikiti wa Swafaa mtaani Kisauni unakuja
baada ya msako mwingine wa Jumatatu ambapo polisi pia walipata silaha gutu
ndani ya msikiti ambao wanasema hutumika kutoa mafunzo yenye itikadi kali.
Mtaa wa Kisauni ndiko vijana waliokuwa wamejihamu kuwadunga
visu watu wanne na kuwaua. Pia waliwashambulia kwa silaha nyingine gutu.
Waziri wa usalama wa ndani, Joseph Ole Lenku anasema kuwa
msako huo ulifanywa katika misikiti ambayo hutumiwa na watu wanaoeneza itikadi
kali za kiisilamu kwa vijana ambao inadaiwa wanajiunga na kundi la wapiganaji
wa kiisilamu la Al Shabaab nchini Somalia.
Viongozi wa kiisilamu wamelanaani misako hiyo katika msikiti
wakisema kuwa itachochea zaidi vijana kuendeleza itikadi kali za kidini.
No comments:
Post a Comment