Pages

Thursday, November 20, 2014

Polisi wanasa silaha zingine Mombasa Kwenye Msikiti

Polisi mjini Mombasa Pwani ya Kenya wanasema wamepata silaha nyingine zaidi ikiwemo mabomu katika msikiti wa tatu ambao ulifanyiwa msako
Msako huo katika msikiti wa Swafaa mtaani Kisauni unakuja baada ya msako mwingine wa Jumatatu ambapo polisi pia walipata silaha gutu ndani ya msikiti ambao wanasema hutumika kutoa mafunzo yenye itikadi kali.
Mtaa wa Kisauni ndiko vijana waliokuwa wamejihamu kuwadunga visu watu wanne na kuwaua. Pia waliwashambulia kwa silaha nyingine gutu.


Waziri wa usalama wa ndani, Joseph Ole Lenku anasema kuwa msako huo ulifanywa katika misikiti ambayo hutumiwa na watu wanaoeneza itikadi kali za kiisilamu kwa vijana ambao inadaiwa wanajiunga na kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Al Shabaab nchini Somalia.

Viongozi wa kiisilamu wamelanaani misako hiyo katika msikiti wakisema kuwa itachochea zaidi vijana kuendeleza itikadi kali za kidini.

No comments:

Post a Comment