KIlabu ya Borussia Drtmund nchini Ujerumani yahofia
kushushwa daraja katika ligi hiyo kutokana na matokeo mabaya msimu huu.
Matokeo mabaya ya kilabu ya ligi ya Bundesliga nchini
Ujerumani Borussia Dortmund yalichukua mwelekeo mpya baada ya kilabu hiyo
kushuka na kuorodheshwa miongoni mwa timu ambazo huenda zikateremshwa katika
ligi hiyo.
Timu hiyo imeshindwa kwa mara ya 10 baada ya mechi 17 msimu
huu na hivyobasi kuwa ya pili kutoka mkiani mwa ligi ya Ujerumani.
Mshambuliaji wa timu ya Warder Bremen Davie Selke na kiungo
wa kati Fins Bartel walifunga bao kila mmoja yaliohakikisha kuwa Borussi
aDortmund inashuka hadi nafasi ya 17 kati ya timu 18.
Mlinzi wa Ujerumani Matts Hummels aliipatia Dortmund
matumaini baada ya kufunga na kichwa.
Licha ya kudhibiti mchezo kwa asilimia 70,Dortmund
ilishindwa kuona lango la Bremen.CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment