Aliyekuwa bingwa wa ndondi ulimwenguni Mohammed Ali amelazwa
hospitalini baada ya kuugua maambukizi ya mapafu.
Ali ambaye ana umri wa miaka 72 na ambaye ana ugua ugonjwa
wa Parkinson anadaiwa kuwa katika hali imara .
Msemaji wake amesema kuwa ugonjwa huo uligunduliwa mapema.
Mohammed Ali wakati wake alipokuwa bingwa wa ndoni duniani.
Hatahivyo hakutoa maelezo zaidi na kutaka haki ya faragha ya familia ya bondia huyo mkwongwe kuheshimiwa.
Ali alipataikana na ugonjwa wa Parkinson mwaka 1984,miaka mitatu baada ya kuustafu katika masumbwi.
Alionekana hadharani katika sherehe moja mnamo mwezi Septemba nyumbani kwake Louisville Marekani wakati wa kutoa tuzo za kibinaadamu za bondia huyo.chanzo BBC
No comments:
Post a Comment