Eneo la mauaji ya polisi wawili mjini New York nchini
Marekani
Maafisa wawili wa polisi mjini New York Marekani wameuawa
kwa kupigwa risasi walipokuwa ndani ya gari lao eneo la Brooklyn.
Kamishna wa idara ya polisi mjini New York Bill Bratton
amesema kuwa maafisa hao walilengwa na kuuawa kutokana na sare walizokuwa
wamevaa.
Alisema kuwa awali mwanamume huyo alikuwa ameandika ujumbe
wa kuwashutumu polisi kwenye mtandao wa kijamii baada ya kumfyatulia risasi na
kumjeruhi vibaya mpenzi wake wa zamani .
Mauaji hayo ya polisi yanajiri wakati kunashuhudiwa ghadhabu
kali kufuatia uamuzi wa hivi majuzi wa kutowafungulia mashtaka polisi wazungu
waliohusika kwemye mauaji ya waamerika weusi.
No comments:
Post a Comment