Hakuna kitu kibaya kama kusahau ulikoegesha gari lako katika
jengo la kuegeshea magari lenye goraf nyingi.
Lakini hivi karibuni hautahihajika kupanda gorofa kutafuta
gari lako kwani kampuni ya kutengeza magari ya BMW, imetangaza kuzindia kifuaa
ambacho kinaweza kuyawezesha magari ya kampuni hio kujiegesha yenyewe kwa
kubonyeza tu kifaa hicho.
Hata hivyo dereva wa gari hilo atalazimika kuvaa saa ya
Smartphone mkononi ambayo ataibonyeza na kuiamrisha kwa sauti gari hilo kwenda
kujiegesha.
Gari hili linaweza kujiegesha lenyewe kwa kutumia saa ya
mkononi ambayo inabonyezwa na dereva
Gari hilo kwa amri ya dereva litatoka liliko baada ya dereva
kushuka na kwenda lenyewe kwa kuhesabu muda utakalichukua kwenda kutafuta
sehemu ya kujiegesha.
Tawi la kampuni ya BMW mjini Munich, Ujerumani limezindua
teknolojia hio ambayo inawezesha gari kujiegesha lenyewe.
Gari hilo linatumia miale ya Leser iliyo kujitafutia ramani
ya jengo ambalo lipo. Dereva anaweza kuliamrisha gari hilo kwenda kujiegesha
kwa kutumia Smartphone.
Dereva anaporejea kutoka alikokwenda, analiamrisha gari
kutoka sehemu ilikojiegesha na kuja kumchukua dereva
Teknolojia hio inajulikana kama ' Remote Valet Parking
Assistant,' na inafanyiwa majaribio kwenye gari la BMW i3.
Badala ya kutumia GPS, teknolojia hio inatumia miale ya
Laser ambayo hutengeza ramani inayolisaidia gari hilo kutafuta sehemu ya kwenda
kujiegesha.
Teknolojia hiyo inaiwezesha gari hilo kuona njia na nafasi
ya kujiegeshea na pia kuona vizingiti mfano kama magari ambayo hayajaegeshwa
vyema.
Kwa mujibi wa waliotengeza gari hilo, linaweza kujitafutia
nafasi ya kujiegesha na hata kuweza kutambua sehemu ambako kuna nafasi.
Teknolojia hio inatengezwa sambamba na teknolojia nyinginezo
zitakazoweza kuzuia gari hilo kugongana na magari mangeine.
No comments:
Post a Comment