Hiyo imekuwa ni mazoea katika maisha ya binadamu
na inachukuliwa tu ni jambo la kawaida lakini ukweli ndani yake kuna
siri kubwa.
Mtu aweza kujiuliza, je, usingizi ni nini na faida
yake ni ipi Ukisoma historia utaona kuwa kwa kipindi kirefu hadi miaka
ya 1950, watu walidhani kuwa usingizi ni hali ya kutokuwa na hisia.
Walikuwa na fikra pia katika usingizi uhai unakuwa
haupo na katika mwili kila kitu husimama na hakuna
harakati yoyote inayoendelea. Hata hivyo, wanasayansi mbalimbali wamefanya tafiti nyingi na kubaini kuwa usingizi unapitia hatua mbalimbali.
harakati yoyote inayoendelea. Hata hivyo, wanasayansi mbalimbali wamefanya tafiti nyingi na kubaini kuwa usingizi unapitia hatua mbalimbali.
Moja ya hatua hizo ni akili kuwa katika hali ya kufanya kazi wakati mwili umepoteza hisia kwa kuwa fofofo kwa usingizi.
Kulingana na tafiti hizo, tunapokuwa usingizini,
ziko hatua tano tunazopitia. Inasemekana kuwa tunatumia asilimia 50 ya
muda wa usingizi katika hatua ya pili, asilimia 20 kwa hatua ya mwisho
na asilimia 30 katika hatua ya kwanza, ya tatu na ya nne. Kwa mtoto
mchanga hutumia asilimia 50 ya muda wa kulala katika hatua ya mwisho.
Katika hatua hizi tano, hatua ya kwanza kunakuwa na hali nyepesi ya usingizi na kuamshwa kunachukua muda mfupi.
Kwa hatua ya pili kuna kupepesa macho na ubongo
hufanya kazi polepole. Hatua ya tatu na ya nne ubongo hupoza kidogo na
ni vigumu kumwamsha mtu kwani anakuwa na usingizi mzito.
Wakati huu macho hayajigusi na mtu akiamshwa huchukua muda mrefu kuwa katika hali yake ya kawaida.
Katika hatua ya tano, hali ya kupumua na mapigo ya moyo huongezeka, shinikizo la damu huongezekana.
Muda wa kulala hutegemea mtu na mtu kutokana na
mambo mengi hasa umri. Watoto wachanga hulala kwa muda wa saa 16 kwa
siku, vijana saa tisa na watu wazima kati ya saa sita na saba, ijapokuwa
wengine hulala saa tano kwa siku.
Wanawake wajawazito kuanzia miezi mitatu ya mwanzo wanahitaji muda mrefu wa kulala
- Mwananchi
No comments:
Post a Comment