Huku wafanyibiashara na wanasiasa wa ngazi za juu wakikutana
katika mkutano wa kiuchumi duniani mjini Davos wiki hii ,hisia tofauti
zimetolewa kuhusiana na kuwepo kwa ukosefu wa usawa duniani bila kuisahau
asilimia moja ya watu Matajiri duniani.
Matajiri hao wanaishi katika visiwa vya kibinafsi,lakini je,
hao ndio matajiri wanaojulikana Pekee?.
Ripoti moja ya shirika la wahisani la Oxfam iliotolewa
sanjari na mkutano huo wa Davos,ilizua hisia kali baada ya kubashiri kwamba
asilimia moja ya matajiri duniani huenda ikamiliki idadi yote ya watu duniani.
Ilitoa utafiti wake kutoka kwa benki ya Credit nchini Uswizi
ambayo inakadiria jumla ya utajiri katika kila nyumba kuwa dola trillioni 263.
Huo ni itajiri na wala si mapato.
Watu matajiri kama vile Bill gates ,Warren Buffet na Mark
Zuckerberg ni miongoni mwa asilimia 1.
Aliko Dangote tajiri mkubwa barani Afrika
Lakini je, ni nani mwengine aliyeorodheshwa katika asilimia
hiyo?.
Kulingana na ripoti hiyo ya benki ya Credit watu wengine
millioni 47 wana utajiri wa dola 798,000 kila mmoja.
Hiyo inashirikisha watu wengi katika mataifa tajiri ambao
pengine wasingejitambulisha kama matajiri,lakini ambao wanamiliki nyumba ama
wamelipa kiwango kikubwa cha mkopo.
Miongoni mwao ni:
Watu millioini 18 wanatoka Marekani
Millioni 4 inatoka Japan
Watu millioni 3.5 wanatoka Ufaransa
Watu millioni 2.9 wanatoka Uingereza
Millioni 2.8 wanatoka Ujerumani
Millioni 4 inatoka Japan
Na millioni 1.6 inatoka China
No comments:
Post a Comment