Twitter
Maelfu ya wanaume nchini Saudia wanajaribu kuwatoa wanawake
katika mtandao wa twitter ,lakini juhudi hizo zinaonekana kuambulia patupu.
Ukandamizaji wa kijinsia nchini Saudi Arabia ni swala la
kawaida na inaonekana baadhi ya watu wanajaribu kulipanua wazo hilo kufika
katika mitandao ya kijamii.
Maneno yaliosema ''hatutaki wasichana katika
mtandao wa
Twitter'' yalitajwa takriban mara 400,000 wikendi iliopita.
Hatahivyo chimbuko la maeneo hayo halijulikani.
Lakini ajenda ya wazo hilo haikufanikiwa kwa kuwa wengi
waliojiunga walikuwa wakipinga ukandamizaji huo wa kijinsia.
Wanawake walijibu nao kwa kusema ''kwa nini? Tumefanya
nini''? .
Mwengine aliandika kwa kusema ''iwapo kungekuwa hakuna
wasichana katika Twitter hakuna mwanamume ambaye angejisajili''.
Wanawake wengine pia walianza kusambaza ujumbe uliosema
''hatutaki wanaume katika twitter'', ili kulipiza kisasi lakini ilipata ujumbe
1,500 pekee.chanzo BBC
No comments:
Post a Comment