Gazeti la Vibonzo la Charlie Hebdo.
Gazeti la kila wiki la vibonzo la Charlie Hebdo la Ufaransa
toleo la kesho Jumatano linatarajiwa kuchapisha kibonzo cha Mtume Muhammad
katika ukurasa wake wa mbele chini ya kichwa cha habari "Yote
yameshasamehewa"
Walioona kibonzo hicho wanasema Mtume Muhammad ataonekana
akishikilia bango lililoandikwa "Je suis Charlie" maneno yenye
tafsiri "Mimi ni Charlie, yaliyotumika kuonyesha mshikamano, baada ya
shambulizi katika ofisi za gazeti hilo Jumatano wiki iliyopita ambapo
wafanyakazi kumi na wawili wa gazeti hilo waliuawa.
Nakala milioni tatu za gazeti hilo la kesho tayari
zimeshachapishwa tofauti na kawaida ambapo huwa linachapisha nakala sitini elfu
kwa wiki.
(CHANZO: BBC SWAHILI)
No comments:
Post a Comment