Mnara wa msikiti mkubwa Afrika
Msikiti utakaoshindana na maeneo mengine ya Kiislam ya
kuabudia makubwa kuliko yote duniani unajengwa katika pwani ya kaskazini mwa
Algeria.
Nini malengo ya kujenga msikiti mkubwa kama huu?
Nusu ya eneo katika ghuba ya Algiers, jengo kubwa taratibu
limeanza kuibuka kutoka ardhini.
Katika sehemu moja kitakuwa chumba cha kuabudia cha Msikiti
Mkuu wa Algiers. Katika sehemu nyingine kutakuwa na mnara mrefu kuliko yote
duniani, ukiwa na urefu wa mita 265 kwenda juu.
Kutakuwa na shule ya korani, maktaba na jumba la makumbusho,
na maeneo na bustani zenye miti ya matunda mbalimbali.
Eneo la ndani
Wageni watawasili katika magari, treni na hata boti. Jengo
hilo, litakalokuwa na uwezo wa kuchukua watu 120,000, litaunganishwa na bandari
katika bahari ya Mediterani katika njia mbili za mandhari ya kutembea.
Msikiti huu utakuwa wa tatu kwa ukubwa wa eneo duniani, kwa
mujibu wa wataalam wa majengo na kuwa msikiti mkubwa kuliko yote barani Afrika.
"Ni moja ya miradi ya karne," amesema Ouarda
Youcef Khodja, afisa mwandamizi katika wizara ya nyumba na mipango miji, wakati
alipotembelea eneo hilo la ujenzi.
Bi Ouarda amesema Rais Abdelaziz Bouteflika alitaka msikiti
huo kuwa"Mnara wa Uislam na kwa mashujaa wa mapinduzi ya Algeria" -
vita vya kupigania uhuru kutoka Ufaransa.
Lakini pia unaamanisha kuwa ishara kwa siku za baadaye.
"Mnara huu utakuwa kitu cha kurejelea katika mapinduzi ya sasa-mapinduzi
ya maendeleo ya Algeria."
Kama ilivyo kwa miradi mingine mikubwa, inayofadhiliwa
kutokana fedha inayotokana na mafuta, ujenzi wa msikiti huu unategemea wataalam
na wafanyakazi kutoka nje. Umebuniwa michoro na wataalam wa majengo wa
Ujerumani na unajengwa na kampuni ya ujenzi ya China iitwayo China State
Construction Engineering Corporation, ambayo ina mamia ya wafanyakazi wanaoishi
katika eneo la ujenzi.
Ujenzi wa msikiti mkubwa afrika
Na kama ilivyo kwa miradi mingine, mradi huu umechelewa
kutekelezwa. Wizara ya nyumba na mipango miji hivi karibuni ilichukua jukumu la
kusimamia ujenzi wa msikiti huo kutoka wizara ya masuala ya dini. "Mungu
akipenda", anasema Bi Youcef Khodja, kwa sasa utakamilika mwishoni mwa
mwaka 2016, japo hata hiyo tarehe, ujenzi utakuwa umechelewa kwa zaidi ya mwaka
mmoja kutoka muda uliokuwa umepangwa.
Vipimo vya msikiti huo, na eneo lake na gharama yake
inakadiriwa kuwa dola za Kimarekani bilioni 1-1.5, ikionyesha kuwa ni
kipaumbele cha serikali.
Sababu moja ya kutekelezwa kwa mradi huu ni uungwaji mkono
na Bwana Bouteflika ambao utakuwa ukumbusho wa urais wake nchini Algeria.
Sababu nyingine inaweza kuonekana kwa ushindani wa mara kwa
mara na majirani zake, Morocco. Msikiti wa Algiers utaupita kidogo msikiti wa
Hassan wa Pili ulioko Casablanca kwa ukubwa wa eneo na kwa urefu wa mnara.
Lakini msukumo mkubwa huenda ukawa jaribio la serikali
kujenga utambulisho wa taifa kidini na kutangaza Uislam kwa kuweka udhibiti juu
ya misikiti na maimam wanaosalisha humo.
Jitihada hiyo iliyoanza pamoja na harakati za uhuru mwaka
1962 na kupata dharura na mgogoro wa kiraia na wapinzani wa Kiislam katika
miaka ya 1990, wakati huo serikali ilipoteza udhibiti wa baadhi ya misikiti kwa
wahubiri waliochochea upinzani dhidi ya utawala wa serikali.
Msikiti mkubwa barani afrika unajengwa na wachina
Ni kwa mantiki hiyo Algeria inajenga msikiti mkubwa wa
kisasa, kitu ambacho kilikuwa kinakosekana mpaka sasa - anasema Kamel Chachoua,
mtaalam wa Algeria wa masuala ya dini katika Taasisi ya Utafiti na Elimu katika
Ulimwengu wa Kiarabu na Kiislam mjini Marseille.
Uamuzi wa kujenga msikiti huu ulikuwa "ukimaanisha
kuwadhibiti wapiganaji wa Kiislam. Ni wazo la kuunda Uislam wa kitaifa baada ya
kitisho cha miaka ya 1990 na kuundolea Uislam taswira mbaya na kuufanya kuwa
karibu zaidi na serikali na kupambana na misimamo mikali ya kidini."
Msikiti huu una maana ya kuwa ishara muhimu katika sehemu ya
Algiers ambayo imeshuhudia vitendo vingi vya misimamo mikali ya kidini katika
miaka ya 1990, amesema.
"ni njia ya kuficha misikiti midogo na kuidunisha. Ni
namna ya kusema: 'Tunapenda Uislam, lakini Uislama wa kisasa'. "Unaweza
kujenga miskiti midogo 1,000 lakini haionekani - haionyeshi kuwa serikali iko
katika mchakato wa kuonyesha udhibiti wake juu ya Uislam na kwamba inajivunia
Uislam."
Wazo la kuhamasisha utaifa wa dini ya Kiislam ambayo
inaondokana na itikadi zenye misimamo mikali kutoka nchi za Ghuba au kwingineko
linaonekana katika jitihada za serikali za kutangaza na kushirikisha Sufi
zawaya, au sheria za kidini. Pia inajidhihirisha katika utaalam wa ujenzi wa
msikiti mpya wa Afrika Kaskazini, wenye mnara mmoja wa muundo wa pembe nne.
msikiti uliopo Algeria
Mnara utakwenda juu ya eneo la Mohammedia, na juu ya mabaki
ya ukoloni uliopita nchini Algeria. Moja kwa moja nyuma ya eneo la ujenzi ni
jengo kubwa lililotumika kukaliwa na wachungaji wa kimisionari kutoka Ufaransa
waliojulikana kama "peres blancs, au white fathers". Chini kidogo ya
barabara ni eneo la kiwanda cha zamani cha mvinyo.
Msikiti huo umebuniwa kuwa ishara ya utambulisho wa Algeria
mpya, lakini utambulisho huo bado unapiganiwa.
Baadhi ya wakosoaji wanauona msikiti huo kuwa zaidi kuwa
ishara ya maelewano baada ya mgogoro na wanasiasa waislam kuliko kuwa njia ya
kupambana na wasilam wenye misimamo mikali.
"Kipaumbele ni kusema: 'Angalia tulivyo nchi ya
Kiislam," anasema Amira Bouraoui, mfuasi wa vuguvugu la upinzani la
Barakat. "Ni njia nyingine ya kuwanyamazisha wapinzani wa Kiislam na
kuwapaka mafuta kwa mgongo wa chupa."
Bi Bouraoui hivi karibuni alitishiwa katika mtadao wa
kijamii wa Facebook baada ya kuuliza kama sauti ya vipaza sauti ingeweza
kupunguzwa. Wananch iwa Algeria wasiofungamana na dini wanaona hili kama
mfululizo wa mifano ya kufuatilia uislam na kukosekana kwa uvumilivu wa kidini.
Hata hivyo kwa kawaida, iwapo Wa-Algeria wanaonekana kuwa
watazamaji zaidi, hiyo ni hali ya juu juu, anasema Nacer Djabi, mwana
sociolojia katika chuo kikuu cha Algiers. "katika kiwango cha kijamii si
fikirii kama wanadini hasa, anasema Djabi.
"Ni watu wasiotaka mabadiliko sana, mabadiliko
wanayoonyesha ni ya juu juu. Unaweza kuona hilo katika mitaa ya Algiers - kuna
wasichana wengi wenye hijab, lakini hizo haziwazuii kuwa na wapenzi wa kiume,
kunywa bia.
"Wa- Algeria wengi, wafanyabiashara, wanakwenda Mecca,
wanaswali mara tano kwa siku", anasema."Lakini hali halibadili tabia
yao kama wananachi kama Waislam."
Kwa upande wao wakazi wa Mohammedia wanaonekana
kutofurahishwa na ujenzi wa msikiti mkubwa katika maeneo yao, wakisema fedha
hiyo ingetumika katika mambo mengine.
"Unatakiwa kuanza na elimu na afya, na baadaye unaweza
kufikiria kuenzi dini," anasema Racim, mwanafunzi mwenye umri wa miaka 22.
"Katika mtazamo wa Kiislam, mahali pa kuswalia si
muhimu sana - ni kile kilichoko moyoni."
No comments:
Post a Comment