Kifaa cha Semenspy
Waswahili husema kwamba siku za mwizi ni arobaini.Msemo huo
sasa huenda ukafanikishwa miongoni mwa akina baba ambao huenda kinyume na ndoa
zao na wabakaji.
Hii ni baada ya kubuniwa kwa kifaa kwa jina Semenspy kilicho
na uwezo wa kubaini majimaji yaliosalia katika chupi,nguo za kulalia,katika
nguo na maeneo mengine baada ya mtu kuhusika katika tendo la ngono.
Kulingana na gazeti la the Nairobian nchini kenya,kifaa
hicho pia kina mwongozo unaofanya mambo kuwa rahisi kwa wanandoa walio na
shauku miongoni mwao.
Maagizo yake ni kwamba iwapo unamshuku mumeo
ama mkeo tafuta
majimaji hayo katika chupi ama nguo zilizotajwa hapo awali.
Kama kifaa cha kupima iwapo mwanamke ni mja mzito Semenspy
kinaweza kubaini mara moja iwapo mtu ana uhusiano mwengine nje.
Kulingana na daktari Wachira wa DIY Solutions,kifaa hicho
kimetengezwa Marekani.Wachira amebaini kwamba amefanikiwa kupata majibu sahihi
kutoka kwa wanawake wanaotaka kujua iwapo waume zao na marafiki zao wa kiume
wanawadanganya katika uhusiano.
Si rahisi kuwakamata wapenzi wanaodanganya kwa kuwa
kunahitaji upelelezi zaidi na subra.
kwa kuwa kuna maji maji ya mbegu za kiume katika chupi ya
mwanamume sio ushahidi kwamba mwanamume huyo anakwenda nje ya ndoa.
Swali ni vile utakavyoonyesha ushahidi kwamba maji maji hayo
yanatoka kwa mwanamume huyo kwa kuwa mara nyingi wengi hutoa maji hayo bila ya
kuhusika katika tendo la ngono.
Daktari Wachira ana shauri kwamba mwanamke anayemchunguza
mumewe anafaa kukaa kwa mda bila kufanya mapenzi, ili kuweza kuchukua sampuli
za maji maji hayo kutoka kwa nguo za mumewe ama mpenziwe.
Anasema kuwa violezi hivyo vinafaa kuchukuliwa mara tatu na
kutoka nguo tofauti za mpenzi anayeshukiwa.
Anasema kwamba si kila mara kwamba maji maji ya mbegu za
kiume humtoka mwanamume bila ya kufanya mapenzi kwa hivyo hhiyo haifai kuwa
sababu ya mwanamume kujilinda.
No comments:
Post a Comment